TUME YA MABORESHO YA KODI, KUNI YA ONGEZEKO LA ULIPAJI KODI WA HIARI
Na Mwandishi, Umoja wa Vijana CCM
Rais Samia Tarehe 04/10/2024 amezindua Tume ya Rais ya Maboresho ya kodi
Kodi ni -mchango wa lazima kwa mapato ya serikali, unaotozwa na serikali kwa mapato ya wafanyakazi ,faida ya biashara, au kuongezwa kwa gharama ya baadhi ya bidhaa, huduma na miamala.
Kodi ni msingi mkubwa kwa maendeleo ya Taifa maana kupitia kodi serikali inalipia huduma zote za umma ambazo watanzania wote tunanufaika nazo, zikiwemo - Hospitali, shule,madaraja ,Ruzuku ,Barabara,hata mikopo ya asilimia 10 za halmashauri inatokana na ukusanyaji wa kodi .
Pia zinawakilisha dhana muhimu kati ya raia na serikali yao kwa msingi wa kutegemeana kwa kuwa hata bajeti za serikali zinategemea asilimia kubwa Kodi za wananchi
Tume Ya Maboresho Ya Kodi , Ni chombo kipya cha Serikali chenye lengo la kushauri,kupitia ,kuboresha na kuweka daraja kati ya Walipa kodi na na mifumo ya ukusanyaji kodi kupitia sheria za kodi zinazobadilika kila mwaka kutokana na mabadiliko ya ki sera ,muundo wa maisha ya kiuchumi na fedha , mahitaji na matumizi ya serikali.
Ulipaji Kodi wa Hiari, Hiki ni kitendo cha mwananchi kushirikiana na serikali yake kwa kuwasilisha marejesho ya kodi ( kipindi husika ) hususani kila mwaka kwa uaminifu na usahihi.
Ikumbukwe: Mei,17 2023 wafanya Biashara Dar es salaam,kariakoo kwenye kikao na waziri mkuu waliomba serikali Iunde tume ya muda kwa ajili ya kupitia malalamiko na mahitaji yao kuhusiana na maswala mazima yahusuyo kodi
Serikali ya Tanzania kupitia Waziri mkuu iliunda tume ya watu 14 kati ya hao saba kutoka kwa wafanyabiashara na saba kutoka serikalini kwa lengo la kupitia changamoto zote zilizo orodheshwa na wafanyabiashara hao . Kitu kilicholeta tija kwa wafanya biashara ,mpaka kupelekea uamuzi wa Rais Samia kuanzisha tume ya maboresho ya kodi yenye tija ya muda mrefu
Mchango wa Tume ya Maboresho Ya Kodi kwenye Ulipaji Hiari wa Kodi
• Itakuwa na msaada wa kuishauri serikali namna bora ya ukusanyaji kodi namna Bora ya kutunga sheria za kulinda na kuratibu mchakato wa kodi wenye tija
• Itasaidia katika kufanya tafiti za kikodi kulinganisha na hali ya Uchumi ili kupanga sera rafiki kwa mlipaji na za mtoza kodi kulingana na mahitaji ya makusanyo
• Ni chombo Kitakachotumika kuwasilisha rasimu ya Mabadiliko madogo ya kikodi kulingana na mabadiliko ya kimazingira na kiuchumi ya walipa kodi
• Kitasaidia kuongeza wigo wa Utoaji Elimu ya mlipa kodi hivyo kutawafanya walipa kodi kuwa na uelewa wa kutosha juu ya wajibu wao kwa serikali inayowaongoza
• Itasaidia kupokea na kuchakata na kuyawasilisha malalamiko ya walipa kodi dhidi wakusanya kodi kwa wasio na ujuzi wa kufikia mahakama za kikodi kuliko kusubiri mpaka viongozi wa ngazi za juu wa nchi
Ushauri kwa Tume ya maboresho ya kodi na Serikali
• Tume iendeleze Tafiti mbali mbali za kikodi na kiuchumi ili kusaidia kupata mangamuzi ya Hatua za kuchukua katika kufanya maamuzi ya kikodi
• Elimu ya Mlipa Kodi Iendelee kupewa kipaumbele kwa vyombo vyote vinanyosimamia maswala ya kikodi na sio kuwaachia mamlaka ya mapato peke yake
• Tume iweke Mapendekezo ya Kutoa adhabu kali inayotekelezeka kwa walipa kodi wanaokwepa kulipa kodi kwa makusudi
• Tume iweke dawati la kupokea malalamiko ya walipa kodi kwa lengo la kupunguza msongamano kwenye mahakama za kikodi ( TRAB &TRAT )
• Tume iendelee kupokea mapendekezo na marekebisho ya sheria za kikodi kutoka kwa Walipa kodi ili kusaidia kuyaweka kwenye utendaji yanayowezekana na kutoa elimu juu ya maoni yenye ukakasi
#Kijananakijani
#samiatunaendanaye2025/30