Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
TUME YA MADINI YATAKIWA KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI KUPAYA TEKNOLOJIA ZENYE GHARAMA NAFUU
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amewaasa Watanzania kutumia fursa za kiuchumi zinazopatikana nchini zikiwemo za kilimo, mifugo, uvuvi na madini katika kujiongezea kipato pamoja na kukuza uchumi wa Taifa.
Kigahe ametoa wito huo wakati akifungua maonesho ya 18 ya biashara ya afrika mashariki yanayofanyika kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Maonesho hayo yanayolenga kutangaza fursa za kiuchumi na uwekezaji mkoani Mwanza na nchini kwa ujumla yameandaliwa na chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) Mkoa wa Mwanza .
Tume ya Madini nchini imeshiriki maonesho hayo ambapo inatoa elimu mbalimbali kwa wananchi ambapo pia mgeni rasmi amezitaka taasisi ikiwemo tume ya madini kuwasaidia wafanyabiashara wakiwemo wajasiriamali kuwawezesha kupata teknolojia zenye gharama nafuu.
Zaidi ya makampuni mia tatu ya kibiashara kutoka ndani na nje nchi yanashiriki kwenye maonesho ya 18 ya biashara ya Afrika Mashariki ambayo yatafikia tamati jijini mwanza septemba tatu, mwaka huu