Tume ya Majeshi ya Kivita [Commission of Armed Forces]

MpigaKura

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2007
Posts
384
Reaction score
101
Amani ya Bwana iwe nanyi;
Papa John Paul II alipoitembelea Tanzania mwaka 1990, Kanisa Katoliki lilimkabidhi Ripoti yenye anwani: Activities of the Church in Tanzania.
Katika ripoti yake hiyo Kanisa Katoliki limetaja kuwapo kwa Tume ya Majeshi ya Kivita [Commission of Armed Forces] ndani ya Kanisa hilo.

Je kuna mwenye data kuhusu tume hiyo?
 
weka hiyo ripoti hapa tuichambue wengine hatujapata kusikia wala kusoma. kama umeisoma basi tuhabarishe zaidi na kama una chanzo chake cha kuaminika kiulize chanzo hicho kikupe nyama zaidi tupate kuelewa
 
1. Hilo jeshi makambi yake yako wapi? kanisani au nje ya kanisa?
2. mkuu wa jeshi ni nani?
3. jukumu lake ni lipi?
4 limesajiriwa au bado kama halijasajiriwa inakuwaje linatangazwa hadharani wakati halina kibali?

5 Je, papa alikuja kulifungua jeshi hilo au lilikuwepo tangu mwanzo?

6 je serikali yetu inajua kuwepo kwa jeshi hili au hapana?
 
Kabla ya kuassume ina maana gani ni vizuri watu wajifunze kwanza. Kusikia "Commission on Armed Forces" haina maana ya jeshi wala chombo cha kusimamia majeshi! Ni chombo cha kuwahudumia kiroho askari wakatoliki kwa kuwahakikishia wanapata huduma mbalimbali za kiroho. Katika nchi nyingine hii huitwa "Military Chaplaincy". Kwa Marekani kwa mfano kuna Jimbo Kuu la Majeshi (Military Archdiocese) ambacho ni chombo chenye hadhi ya Jimbo kinachohudumia wanajeshi wa Marekani ambao ni wakatoliki mahali popote walipo.

Kwa Tanzania Kanisa Katoliki kinatumia Commission for Armed Forces kutoa huduma za kiroho wakati wa vita, majanga na makambini. Ikitokea vita kwa mfano mapadre wanaweza kuambatana na wapiganaji kwa ajili ya huduma za kiroho. Jambo hili si geni na karibu nchi mbalimbali zinazo taasisi hizi na Marekani na Uingereza zimeanza hata kuajiri Maimamu kama Military Chaplain kwa ajili ya huduma za kiroho za Waislamu ambao wanatumikia majeshi.

Kwa ufupi, hata Waislamu wanaweza kuanzisha chombo ambacho kitatoa huduma za kiroho kwa wanajeshi. Wanaweza kuita Islamic Commission for Armed Forces. Hatutafikiria wameamua kuanzisha jeshi! Na kwa ufupi tafrisi ya "armed forces" siyo "majeshi ya kivita"!
 

Mkuu,

Kwa hapa Tanzania je hiyo commission inafanya kazi hiyo sasa?

Je commission hiyo wakati wa vita na Uganda ilikuwa inawahudumia wakatoliki kiroho tu??

Je walio ruhusu mtindo huo kuwepo katika jeshi letu walifikir taifa ni la kikatoliki tu...

sipati picha kuwafundisha wanajeshi ukatoliki wakati mission ya jeshi ni kulinda nchi na si kulinda ukatoliki
 

Kama nilivyoeleza hapo juu haikueleweka kwa kweli siwezi kukusaidia.
 
Kama nilivyoeleza hapo juu haikueleweka kwa kweli siwezi kukusaidia.

Mfumo kristo hadi jeshini; huwezi kueleweka..kwani kuna ugumu gani hapo?

Je walipokuwa wanapigana vita uganda wanajeshi wa kiislam walipata huduma za kiroho kutoka association gani?

Je hapo viongozi wa kiserikali hawakuona kuna mushkeli (kama kweli wapo kitaifa na si kikatoliki zaidi??)
 

Nilichokieleza hapo juu siyo kigumu hivyo kuelewa na wala hakijaelezea juu ya uwepo wa chaplains wakati wa vita ya Uganda. Sasa, kwa kweli sina namna ya kukusaidia kwa kweli. Nimejaribu kuelezea ni nini hiyo. Ukitaka kujua zaidi kazi zake au historia yake TZ unaweza kufuatilia TEC. Sina ujuzi wowote kama Tume hii inamapadre au mashemasi wanaofanya kazi moja kwa moja kwenye majeshi kama walivyo machaplain wa nchi nyingine.

Siwezi kushangaa vile vile kama BAKWATA nao wanao mashehe au maimamu ambao wanaruhusiwa kwenda kufanya ibada au kuongoza ibada na swala mbalimbali kwenye makambi ya kijeshi. Haitanishangaza.
 
MM. Kaka umeweza kutanabaisha ukweli kuhusu hii phenomenon kama ambavyo mtoa mada wa awali alivyokua in crossroad. Thanks.
Labda kwa wengine swala hapa sio kusuccumb military operations kwenye dini lah hasha! Ni kwamba kwenye operatios maalum kama vile vita,pale kuna jamii inayohitaji huduma za ki-imani katika mazingira flaniflani. Mfano mzuri ni kwamba UNHCR wanapohudumia wakimbizi wanaheshimu uwepo wa huduma hii kwenye host community. Inatokea kwa mfano mkimbizi anakaribia kuaga dunia (kutokana na kuumwa ama sababu yeyote) kulingana na imani yake ndugu ama mwenyewe anaweza kuagaiza kupata huduma za mwisho za ki-imani. Najua Catholic wanahuduma ya upako- sijui kuielezea lakini nimeshawahi kushiriki mara nyingi zaidi. Hivyo basi vitani ama kwenye risky operation kama hizi za kijeshi hii placement ni ya kawaida kabisa. Cha kukumbuka ni kwamba huduma hii haiathiri uwepo wa imani zingine za dini na sio lazima kwa mtu ambaye anaona hakuwa na wito. MM thanks
 

Tuwaulize BAKWATA kama wanatoa huduma ya kiroho kwa wanajeshi wakiwa katika operesheni zao zenye risky kubwa ya maisha
 
Huu ni mtindo wa kiroho ambao upo kwenye nchi nyingi duniani.
 
"Champlaincy Ministries" au kwa kiswahili "Champlensia" katika taasisi za dini sio jambo geni, hii ni huduma za kiroho katika maeneo mahususi katika jamii na hasa katika taasisi zifuatazo:

1. Taasisi za elimu (kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu)
2. Majeshini (majeshi ya kivita na yale yasiyo ya kivita)
3. Magereza
4. Hospitalini
5. Baadhi ya taasisi muhimu kama vile Bunge au Ikulu.

Kwa hapa Tanzania labda ni huduma zile za kiroho zitolewazo hospitalini, magereza na katika taasisi za elimu pekee. Sijawahi kusikia kuwa kuna chaplain Bungeni (Kwa ajili ya wakristo na waislam). Ila kule US katika tasisi zote hizo kuna Chaplains.

Ambaye hajaelewa maelezo ya mwanakijiji, aende kwa kiongozi wake wa dini amuulize atajulishwa.
 

asante sana kwa maelezo mazuri na yanayojitosheleza................. big up mkuu..................

Kama nilivyoeleza hapo juu haikueleweka kwa kweli siwezi kukusaidia.

hata miye nashangaa iweje kwa maelezo yale bado hajaelewa.................... inaonekana mwenzetu anasoma post huku tayari anayo majibu au assumptions zake kichwani.................. sasa akipewa uelewa wa jambo alilokuwa halijui, yeye anaona kuwa jibu halieleweki.................... hahahaaa.................... kazi kwelikweli.........................

Mwenye ujuzi wa kina kuhusu hii tume ya majeshi ya kivita atujuze...

kwa kweli kama hujamwelewa MM .......................... basi tena mkuu..................sijui nani atakuelewesha vizuri zaidi ya hapo....................


mkuu .....................big up kwa maelezo mazuri ya ziada................. kwa hapa kwetu TZ, champlensia zipo mashuleni/vyuoni (mfano chuo kikuu; wakatoliki, walutheli na waislamu wote wanazo pale)................... magerezani, ......................... na bungeni (waislamu)................... mahospitalini (mfano muhimbili nk)...................

kama hujaelewa, tembelea chuo kikuu (mlimani), ...............gereza lolote lililo karibu, ................ofisi za bunge ...................na hata hospitali ya muhimbili utapewa maelezo juu ya hizo champlensia na zinavyofanya kazi..................... na kama zinachochea udini kwenye taasisi hizo, pia usisahau kuuliza.................. bila shaka watakuambia............
 

nimeosoma hii thread but nlichoona ni kwamba hakuna aliyejibu sahihi. hata mwanakijiji hajajibu sahihi pia,sasa sijajua kama hana jibu sahihi kwa nini alijibu,may be aliona ingeleta kitu fulani lakini ukweli unabaki hiyo ni tume ya majeshi, ya commision OF armed force, yani ni kikosi cha jeshi kinachoongozwa na commander ambaye kikosi kinapata order kutoka kwake! na hii commision ipo ndani ya JWTZ,yeye MWANAKIJIJI kasema Commision ON armed forces! na hajajibu sahihi kabisa yani mbingu na ardhi, ila amejitahdi ili isionekane hamna jibu. (a perplexing
revelation made in an official report
by the Roman Catholic church in
Tanzania and submitted to Pope
John Paul II when he visited
Tanzania in 1990. In its report titled
Activities of the Church in Tanzania the
Catholic church has reported about
the existence of a Commission of
Armed Forces within the church.
The report is silent about when that
Armed Forces Commission was
established within the Catholic
church in Tanzania ). Hivi tujiulize kweli si tunasema humu ni jamii intellgnce, najua kuna watu wanajua na wengne wameelewa ila wengne wameamua kunyamaza. na wengne wako biased may be inagusa imani yake na anaona hatia kwamba kuna udini,ni kweli inawezekana wewe hupendi udini lakini kuna mtu anamamlaka kwako anaendeze, lakini kuna usemi unasema, SEMA KWELI JAPOKUWA CHUNGU. lets be frank pals na tuache kuzinafiki nafsi zetu na ukwel tunaujua!
 
nadhani ni ishu ya uamuzi kama huku wameamua basi hata Bakwata na denomination nyingine zinaweza kuamua peleka watoa huduma wao katika sehemu kama hizo...
 
It is a pit that we have people of this understanding in the forum.
To help you understand the Catholic church, and how its work towards mankind is organized, see this.

 
Nakushauri upate nafasi ya kujifanyia retreat!!!
you really really need to assess yourself!! You have got big problems za uwelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…