Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,581
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amezindua tume maalumu aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na kuwataka wajumbe wake watafute kiini cha kuporomoka kwa ufaulu kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.
Pamoja na nia nzuri ambayo Waziri Mkuu Pinda anayo, katika suala la kuunda tume amefichua siri ambayo bila shaka itaibua makubwa zaidi kwa Watanzania.
Haijulikani ni kwa bahati mbaya au kwa makusudi, huenda ni Pinda au washauri wake ndio waliomwambia aseme haya.
Lakini alichokisema ni cha kweli, kama ni cha kweli basi tukiri kuwa Pinda ni muungwana na amethibitisha pasipo shaka kuwa tangu serikali ya awamu ya nne iingie madarakani, elimu imekuwa ikishuka mwaka hadi mwaka.
Bila hofu yoyote, Waziri Mkuu alisema: Katika suala hili ilibidi tuanze kuchunguza matokeo ya tangu mwaka 2005 hadi 2012, tulijikita katika kuangalia shule zote, katika maana ya shule za wananchi, shule za watu binafsi, shule za serikali ambako huwa tunapeleka mkono, na shule za seminari, zile ambazo huwa ni washidani wetu.
Waziri Mkuu kwa kauli yake anasema: Nimetafuta takwimu za tangu mwaka 2005, Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani na kubaini kuwa tangu wakati huo hadi mwaka 2009 tulikuwa tukifanya vizuri, lakini kuanzia mwaka 2010 hadi 2012 matokeo yamekuwa yakishuka sana.
Pinda alisema hayo akiwaambia wajumbe wa tume hiyo na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema: Mwaka 2005 kiwango cha ufaulu kilikuwa asilimia 89.3; mwaka 2006 asilimia 89.12; mwaka 2007 asilimia 90.6; mwaka 2008 asilimia 83.6 na mwaka 2009 asimilia 72.5, mwaka 2010, kiwango cha ufaulu kilishuka na kufikia asilimia 50.4, mwaka 2011 kilipanda kidogo na kufikia asilimia 53.6 na kilishuka zaidi mwaka jana ambapo kilifikia asilimia 43.5. Hapa ni lazima mtu utapata maswali ya kujiuliza nini kimetokea.
Ukifuatilia takwimu za ofisi ya waziri mkuu, maana yake ni kuwa tangu Serikali ya awamu ya nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete iingie madarakani, elimu imekuwa ikishuka kila mwaka, kasoro mwaka 2007 tu.
Je, Waziri Mkuu alikuwa anakiri kuwa serikali iliyopo madarakani haithamini elimu, au alikuwa anaonesha kuwa imeshindwa?
Hii sio bahati mbaya, takwimu hizi hakuombwa azitoe, yeye alihusika na tume ya taifa ya kuchunguza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012, kutaja takwimu za miaka yote ambapo serikali ya awamu ya nne imekuwa madarakani, tena zisizovutia, ni aibu.
Kila mara tunalalamika kuwa ufaulu umeshuka, kiwango cha udanganyifu kimepanda. Hili limekuwa tatizo linalohitaji hatua kuchukuliwa.
Mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiongea nami wiki hii, alisema suala la matokeo mabovu ya kidato cha nne, halihitaji kuundiwa tume. Alisisitiza kuwa matatizo ya kufeli kwa wanafunzi yanajulikana.
Nilipoongea na mhadhiri huyo, nilifikiri kweli serikali haijui matatizo hayo ndiyo maana inaunda tume. Lakini tamko la Waziri Mkuu kwa maandishi linaonesha kuwa serikali inayajua matatizo yaliyosababisha watoto kufeli, lakini badala ya kutatua ikaamua kuunda tume.
Waziri Mkuu ameamua kukubali tume ikaangalie mitaala na mihutasari, lakini ikumbukwe kuwa yeye pamoja na wabunge wa CCM ndio waliokataa kujadili hoja hiyo bungeni ilipopelekwa na James Mbatia (Mbunge wa Kuteuliwa na Rais).
Wakakubali Watanzania tuoneshwe mitaala feki ambayo waziri mhusika na elimu alishindwa hata kuonesha nakala moja.
Maswali mengi yanaibuka katika hoja hii. Kama suala ni kuangalia mitaala, kwanini serikali ilikataa hoja ya Mbatia? Hapa ninanusa harufu kuwa Waziri Mkuu alishiriki kuhujumu hoja hiyo ili aitekeleze kwa mtazamo anaotaka yeye.
Pili, Waziri Mkuu anawataka wajumbe wa tume kutathimini umahiri wa walimu kumudu maudhui ya masomo wanayofundisha.
Je, ina maana serikali inatilia shaka uwezo wa walimu? Je, ikigundua hawana uwezo ipo tayari kuwapeleka shule? Kama hawana uwezo waliajiriwa vipi? Na je, wamekuwa hawana uwezo mwaka huu kwa kuwa wanafunzi wamefeli? Serikali imewaangaliaje walimu katika kila wanachodai?
Waziri Mkuu anataka tume ikaangalie mazingira ya kufundishia. Hivi ni kweli serikali haijui kuwa shule hazina madarasa, madawati, vifaa vya maabara hadi iunde tume kuchunguza?
Pamoja na hayo Waziri Mkuu anaitaka tume ikaangalie utoshelevu wa walimu. Maana yake serikali haijui kama walimu ni pungufu katika shule? Nimeshindwa kuelewa dhana ya serikali na tume hii. Hadidu hizi za rejea zinaonesha kama vile hatupo makini au tunafanya utani.
Vitu vinavyoonekana tunafanya kama vile havionekani, na vile visivyoonekana tunafanya kama vile vipo hadharani.
Waziri mkuu anaitaka tume kuoanisha utungaji wa mtihani na mihutasari iliyotumika kuwaandaa wanafunzi.
Katika hoja hii, kama mihutasari yenyewe ilikuwa ina utata bungeni, mahali ambapo ingetolewa kwa wabunge wawakilishi wetu kwa uwazi, ilishindikana, huku mtaani kwa tume ya watu kumi na tano tu inawezekana?
Ilishindikana mihutasari halisi kuoneshwa bungeni. Iliyooneshwa ilisemekana ina makosa, ilikuwa mihutasari ya bara tu, haikuhusisha Zanzibar.
Tume ina watu kutoka Zanzibar ni kweli. Je, upimaji huu unaotakiwa na Waziri Mkuu utazingatia mihutasari ipi? Ile iliyokuwa na makosa ya uchapaji au ile ambayo haikuwepo, ambayo Mbatia aliidai serikali ikashindwa kuoneshwa? Au itatengenezwa mingine ili kuweza kukidhi mahitaji ya tume? Maswali haya yanazidisha utata.
Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Gratian Mukoba, wiki hii amenukuliwa akisema kuwa yeye haoni umuhimu wowote wa tume hiyo, akashauri kuwa pesa ambayo ingelipwa kwa tume hiyo ya watu kumi na tano, na wajumbe toka sekretarieti wanaotoka ofisi ya Tamisemi na Wizara ya Elimu ilipwe kwanza madeni ya walimu.
Katika mazingira haya ambayo walimu wanaona wanaidai serikali haiwalipi, badala yake inaunda tume kwa masuala yanayoonekana. Je, walimu watatoa ushirikiano kutafuta ufumbuzi kwa suala hili?
Kauli ya Rais wa CWT kutokubaliana na tume ya kuchunguza matokeo, na yeye kutoteuliwa akateuliwa msaidizi wake, je atatenda kinyume na maoni ya kiongozi wake?
Je, yupo tayari kuwasaliti walimu wenye madeni makubwa waliorudishwa kwa nguvu na mahakama bila kusikilizwa? Hili nalo bado linazidisha utata.
Wakati anahitimisha, Waziri Mkuu aliwataka wajumbe wa tume wafanye haraka ili ikiwezekana waliofeli warudie mtihani, na akaongeza kuwa walimu wastaafu wa sayansi wanaweza kurudishwa kazini ili kusaidia kuondoa upungufu huo.
Walimu waliopo kazini wanadai madeni kibao, waliostaafu bado wanazungushwa pensheni zao na madai mbalimbali kwa serikali yao. Je, wastaafu hawa wanaweza kuwa tayari kuja kuendelea kufundisha? Hela yao itapatikana wapi wakati wale waliopo kazini hawajalipwa?
Na huu utaratibu wa kuwarudisha waliofeli ili wafanye mtihani, kwa kuwa serikali imeona kuwa inaaibika, je, haitaweza kuwarudisha hata wale ambao hawana uwezo ili waonekane wote wamefaulu?
Tume hii inawezekana imeundwa kwa nia nzuri, ila imeibua vitu vingi zaidi.
Juzi, Kenya ilitangaza matokeo yake, ikasema udanganyifu katika mitihani hakuna, kiwango cha ufaulu ili wanafunzi waende elimu ya juu ni asilimia mia, na watu 88 wamefungwa kwa kukiuka sheria mbalimbali katika mitihani.
Tujipime tujilinganishe na wao tuangalie tumekosea wapi? Visingizio vya tume havitaleta suluhisho la kudumu, lakini pia hadidu za rejea zitaendelea kuumbua utendaji wa Serikali ya Kikwete.
SOSI:TANZANIA DAIMA
MY TAKE:MOJA YA TATIZO LA ELIM TANZANIA NI HILI,HII NI SHULE