Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi: Tunataka mfumo wa kodi uwe rafiki kwa walipakodi, uimarike kwa uwazi

Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi: Tunataka mfumo wa kodi uwe rafiki kwa walipakodi, uimarike kwa uwazi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi imefanya kikao na wadau wa kodi mkoani Iringa, ikilenga kupokea maoni na mapendekezo kuhusu changamoto za kodi na tozo mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya biashara.

Mjumbe wa Tume na Mwenyekiti wa kundi dogo la Tume, Balozi Mwanaidi Maajar, amesema kuwa lengo la mikutano hiyo ni kuhakikisha mfumo wa kodi unakuwa rahisi, wa haki, na wenye kuchochea maendeleo.

“Tunataka mfumo wa kodi uwe rafiki kwa walipakodi, uimarike kwa uwazi na usaidie kukuza biashara badala ya kuzuia maendeleo. Ushirikiano wenu wadau ni muhimu kufanikisha haya,” amesema Balozi Maajar.

 
Back
Top Bottom