Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Zanzibar litaanza tarehe 07 hadi 13 Oktoba 2024.
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika Kisiwani Pemba, Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk, alieleza kuwa zoezi hili litafanyika katika mikoa ya Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba.
Uboreshaji huu ni sehemu ya mzunguko wa sita wa zoezi la uandikishaji kwa upande wa Zanzibar, na lengo kuu ni kuwaandikisha Watanzania wote wanaoishi Zanzibar ambao wanastahili kujiandikisha ili kushiriki katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Soma pia: Uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura wakamilika rasmi mkoani Dodoma na Singida
Mjumbe wa Tume, Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari, alieleza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 ya mwaka 2024, Tume itaandikisha Watanzania wote waliotimiza umri wa miaka 18 au watakaotimiza umri huo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Aliongeza kuwa ili mtu aweze kuandikishwa, lazima awe hajapoteza sifa zake kwa mujibu wa sheria na awe na haki ya kisheria ya kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Watanzania wanaoishi Zanzibar lakini hawakufuzu kujiandikisha kupitia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) watapewa nafasi ya kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano pekee.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura liliazinduliwa rasmi tarehe 20 Julai 2024 mkoani Kigoma na limeendelea katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Singida, na baadhi ya maeneo ya Dodoma.