nivoj.sued
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 221
- 190
Wana JF:
Mwaka 2010 Makao Makuu ya Chadema yalipeleka orodha ya wagombea udiwani viti maalum katika Tume ya Uchaguzi ili kuiwezesha Tume hiyo kuteua madiwani wa viti maalum kwa ajili ya Halmashauri mbalimbali ikiwemo Karagwe.
Wakati Makuu ya Chadema yanaandaa orodha hiyo, walikuwa na seti mbili za majina ya wagombea udiwani (viti maalum) kutoka Karagwe. Seti moja ilikuwa halali kwani ilipatikana kwa mujibu wa vikao halali vya chama wilayani Karagwe vilivyoongozwa na Katibu halali wa Wilaya (Deus Rutakyamirwa). Deus Rutakyamirwa alikuwa katibu halali kwa kuwa alikuwa ameteuliwa rasmi na Katibu mkuu wa Chama kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.
Na seti ya pili ilikuwa haramu kwani ilipatikana kwa mujibu wa vikao haramu vya chama wilayani Karagwe vilivyoongozwa na Katibu haramu wa Wilaya (Linus Kishenyi). Linus Kishenyi alikuwa katibu haramu kwa kuwa hakuwa ameteuliwa rasmi na Katibu mkuu wa Chama kwa mujibu wa Katiba ya Chadema. Badala yake alifanikiwa kupata barua tata iliyomtambua na kumtambulisha kama Katibu wa Wilaya ya Karagwe. Barua hiyo ilisainiwa na Victot Kimesera kwa niaba ya Katibuy Mkuu.
Kwa kuwa Katibu haramu wa Wilaya ya Karagwe (Linus Kishenyi) alikuwa na wenyeji wake Makao Makuu ya Chadema, orodha yake haramu ndiyo iliyopelekwa Tume ya Uchaguzi. Uongozi halali wa Chadema Wilayani Karagwe ulipata taarifa kuhusu jambo hili na hivyo kuueleza uongozi mkuu wa Chadema kuhusu manunguniko yao. Uongozi ulichukua hatua za kuiandikia Tume kuiomba isitishe uteuzi wa madiwani viti maalum Karagwe ili kwa njia hiyo chama kipate muda wa kuwasilisha orodha sahihi. Barua kwenda Tume ilisainiwa na John Mnyika kwa niaba ya Katibu Mkuu.
Baadaye kidogo, Tume ilipofanya uteuzi wa madiwani, watu wa Karagwe wakapata diwani ambaye ametokana na vikao haramu vya chama Wilayani humo. Diwani huyo ni Juliet Lushuli. Kwa sababu ya uteuzi huu ilikuwa imefahamika kwamba Tume haikuzingatia ombi la Chadema, yaani ombi la kupatiwa muda wa ziada ili iweze kuwasilisha orodha halali ya wagombea.
Hivyo, Baraza la Mashauriani la Wilaya lilikaa Machi 04, 2012 chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu (Slaa) ili kujadili dosari hii. Kikao kiliridhika kwamba kweli Juliet Lushuli hakuwa ametokana na ridhaa ya vikao halali. Naye alihudhuria kikao hiki. Hivyo, alishauriwa na kikao kujiuzulu na akafanya hivyo. Kwa sababu hii nafasi ya udiwani viti maalum Wilayani Karagwe kupitia Chadema ikawa wazi, na ni wazi mpaka leo.
Kikao hicho kiliagizwa na Katibu Mkuu (Slaa) kuandaa orodha sahihi ya wagombea udiwani (viti maalum) na kuiwasilisha kwake. Hatimaye angeiwasilisha orodha hiyo mpya katika Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya utezi mpya wa diwani halali.
Taarifa zinaonyesha kwamba, mwishoni mwa Oktoba 2012 Tume ya Uchaguzi imekiandikia Chama cha Chadema kwamba nafasi ya Udiwani Viti Maalum (Karagwe) kupitia Chadema iko wazi, na kwamba mtu anayepaswa kurithi nafasi iliyoachwa wazi na Juliet Lushuli atakuwa ni Selina Nguma.
Kwa hiyo Tume ya Uchaguzi imeutaka uongozi wa chama utoe taarifa kuhusu status ya Selina Nguma kichama ili kama bado anazo sifa aweze kutangazwa kama diwani viti maalum Karagwe. Tume inasema kwamba Selina Nguma atakuwa amepoteza sifa ya kuteuliwa endapo mojawapo kati ya yafuatayo limetokea: (1) Amehama Chama, (2) Amefukuzwa Chama, au (3) Amekuwa kichaa na kuthibitishwa na Daktari.
Tume imejizuia kusema kwamba Selina Nguma anaweza kuwa amepoteza sifa endapo ametokana na orodha iliyopatikana kinyume cha taratibu za ndani ya chama. Na kwa kweli, huyu Selina Nguma ni miongoni mwa watu walio kati orodha haramu ya wagombea udiwani viti maalumyaani orodha iliyoandaliwa na Katibu haramu Linus Kishenyi.
Kwa hiyo, kama atateuliwa kama diwani viti maalum, sababu ile ile iliyowafanya watu wa Karagwe kumkataa Juliet Lushuli inapaswa kutumika kumkataa Selina Nguma. Na kama watu wa Karagwe wakilazimishwa kumkubali Selina Nguma basi Karagwe watakuwa wamepata diwani ambaye hakutokana na ridhaa yao.
Selina Nguma atakuwa ni diwani aliyetokana na makosa ya Uongozi wa Makao Makuu ya Chama na/au shinikizo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba Tume hii imekataa kupokea orodha mpya ya wagombea udiwani kutoka Karagwe kwa kuwa orodha hiyo ni time-barred kisheria.
Katika hali ya aina hii sheria inasemaje kuhusu haki ya watu wa Karagwe kupata diwani aliyetokana na ridhaa yao? Naomba ushauri kutoka kwa Wana-JF.