Pre GE2025 Tume ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza kuanza kuandikisha wananchi kwenye daftari mkoani Songwe, Njombe, Rukwa na Ruvuma kuanzia Januari 12

Pre GE2025 Tume ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza kuanza kuandikisha wananchi kwenye daftari mkoani Songwe, Njombe, Rukwa na Ruvuma kuanzia Januari 12

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wanabodi,

Baada ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kufanyika Dodoma na viunga vyake sasa zoezi limehamia mikoa mingine

====================================================
Kupitia ukurasa wa Instagram wa INEC, tume hiyo ya Uchaguzi imetangaza kuwa uboreshaji wa daftari utafanyika kwa wakati mmoja kwenye mikoa ya Songwe, Njombe, Rukwa na mkoani Ruvuma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Mbinga, Mbinga Mji, Wilaya ya Songea na Manispaa ya Songea, kwa siku saba

Zoezi litaanza kuanzia tarehe 12 hadi 18 Januari, 2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Wana Ruvuma na Songea msijifanye hamjaona ujumbe kutoka kwenye tume huru ya Uchaguzi nendeni mkajiandikishe

 
Gharama na sarakasi zote hizi za nini wakati uchaguzi Ukifika tayari hiyo tume Ina matokeo baada ya kuengua wapinzani na kuhesabu kura hewa!
A waste of time and money hakutakuwa tofauti yoyote ya uchaguzi ujao na ule wa mkwe Mchengerwa
 
Wahamiaji haramu wengi hutumia fursa hii kupata hiki kitambulisho na wanakitumia kama kitambulisho cha ukaazi.

Nimeenda nchi kadhaa za Africa Mashariki mimekuta watu wana hivi vitambulisho kwenye nchi zao. Huwa wanajazana tanzania vipindi kama hivi vya kujiandikisha.


Nilikuwa Burundi tuluvyofika mpakani nikaona warundi wengi wanaishi Dar es salaam wametoa vitambulisho vya kupigia kura kama watanzania na wakawa wanadai wapewe barua za ujirani mwema. Ila kimsingi sio watanzania na walikuwa wanaongea kwenye gari wakidhani na Mimi ni mmoja wao. Kwa dizaini hii tutakuwa na wahamiaji haramu wengi.
 
Back
Top Bottom