Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mwenyekiti Tume huru ya Taifa ya uchaguzi, Jaji Mbarouk S. Mbarouk amesisitiza kuwa ni kosa kisheria mtu mmoja kujiandikisha jina lake la kupiga kura zaidi ya mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
Mbarouk ameyasema hayo leo 15 Desemba 2024 katika uzinduzi wa mkutano wa tume na Wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura uliofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Mbarouk ameongeza kuwa zoezi la kujiandikisha kama mpiga kura linapaswa kufanyika kwa uangalifu na kwa kuzingatia sheria zilizopo.
"Ni kosa kubwa kisheria kwa mtu kujiandikisha mara mbili au zaidi na endapo ikitokea hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaoshirikiana katika vitendo hivyo na Ikumbukwe kuwa uchaguzi ni mchakato wa haki na tutahakikisha kuwa hakuna mtu atakayekosa haki ya kupiga kura wala mtu yeyote atakayejihusisha na udanganyifu", amesema Mbarouk