Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Hivi sasa kumezuka kampeni zisizo rasmi zinazofanywa na viongozi wa serikali na wa mashirika ya umma, kampeni hizi zimelenga eti kutatua matatizo ya wananchi ikiwa ni kutoa misaada na mikopo! Huu ni wakati wa kampeni za uchaguzi hivyo kampeni hizi zinaingiliana na kampeni rasmi.
Chaguzi zilizopita hazikuwahi kuingiliwa kwa kiasi hiki ambapo mgombea wa upinzani akitoa ahadi basi kesho atajitokeza viongozi wa serikali na kuanza kutatua tatizo hilo! Huu si mtindo mzuri kwenye wakati wa uchaguzi kwani baadhi yake ni rushwa za waziri kama kilichofanyika huko Mbeya kwa kutoa mikopo ya bajaji wakati huu.
Tume ya uchaguzi na TAKUKURU simamieni uchaguzi kufuatana na sheria na kanuni zake.