Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi: Tunasubiri tangazo la kuvunjwa kwa Bunge ili tutangaze tarehe rasmi ya Uchaguzi 2020

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inasubiri tangazo kwenye gazeti la Serikali la kuvunjwa kwa Bunge ili iweze kuweka tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu.

Mkurugenzi wa NEC, Dkt. Wilson Mahera amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Arusha na kusema baada ya tangazo hilo tarehe itatangazwa.

Amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu 37(1) kinaielekeza Tume kufanya uteuzi kwa wagombea nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani.

Pia, amesema sheria hiyo kifungu cha 46 (1) kinaelekeza kuwa tarehe ya uteuzi wa wagombea itatakiwa kutajwa ndani ya siku 60 hadi 90 kabla ya kutangazwa siku ya uchaguzi.
 
Inamaana hawakuona ile hotuba ya mzee baba alivyojipinda kuelezea Mambo yote yale na kuvunja bunge bado wanasubiri tangazo..!!

Dah! Kweli zimwi likujualo halikuli likakwisha
 
Kwahiyo wameeeishia kujimwambafai Dodoma na kula ubwabwa kisha wakasahau kufanya legal procedures?

Kuwa kwa miaka mitano hadi samaki nao wameomngezeka urefu, madini yameongezeka. Karibu karanga
 
Inamaana hawakuona ile hotuba ya mzee baba alivyojipinda kuelezea Mambo yote yale na kuvunja bunge bado wanasubiri tangazo..!!

Dah! Kweli zimwi likujualo halikuli likakwisha
Sheria
 
Hilo ni takwa la kisheria.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inasubiri tangazo kwenye gazeti la Serikali la kuvunjwa kwa Bunge ili iweze kuweka tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu.

Mkurugenzi wa NEC, Dkt. Wilson Mahera amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari jijini Arusha na kusema baada ya tangazo hilo tarehe itatangazwa.

Amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu 37(1) kinaielekeza Tume kufanya uteuzi kwa wagombea nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani.

Pia, amesema sheria hiyo kifungu cha 46 (1) kinaelekeza kuwa tarehe ya uteuzi wa wagombea itatakiwa kutajwa ndani ya siku 60 hadi 90 kabla ya kutangazwa siku ya uchaguzi.

Kuna watu wanasema wabunge wasiage kwani ni watu wa kawaida sio wabunge tena. Kumbe tangazo rasmi la kuvunja bunge bado!

Cc: Zygot, yehodaya, nawatafuna
 
Inamaana hawakuona ile hotuba ya mzee baba alivyojipinda kuelezea Mambo yote yale na kuvunja bunge bado wanasubiri tangazo..!!

Dah! Kweli zimwi likujualo halikuli likakwisha
Ujue katiba na sheria vinaelekezaje usiwe juha!
 
Inamaana hawakuona ile hotuba ya mzee baba alivyojipinda kuelezea Mambo yote yale na kuvunja bunge bado wanasubiri tangazo..!!

Dah! Kweli zimwi likujualo halikuli likakwisha
Ungehifadhi ufahamu wako mbele ya kadamnasi kwa hili.
 
Back
Top Bottom