Jamii ya udom imeingiwa na hofu kutokana na tetesi za tume ya uchaguzi wa serikali ya wanafunzi hasa katika kitivo cha sayansi ya jamii kuingia katika mgogoro mkubwa na utawala juu ya uchaguzi huo,tangu tume hiyo ianze kazi tarehe 12/04/2013 mpaka sasa licha ya hali ngumu na sintofahamu iliyogubika,inasemekana kuwa tume hiyo imekuwa ikijiongoza kwa kutumia michango ya wajumbe,hii imetokana na utawala kuingilia maamuzi ya bunge na rais kuhusu bajeti ya tume hiyo,imeelezwa kuwa tatizo hilo limesababishwa na kaimu mshauri wa wanafunzi madam aziza! Mpaka sasa tume imeratibu zoezi zima na majina ya wagombea yametoka licha ya hali hiyo ngumu,hapa social sciencies kumepoa na hatima ya wanafunzi kuwachagua viongozi wao haijulikani: Suala la aziza kuingilia zoezi hili limewakasirisha wengi na kuwafanya wanafunzi kutokujua hatima ya uongozi wao: Kutokana na matatizo ya kuingiliwa kwa tume hii pamoja na kunyimwa bajeti,kuna tetesi kwamba tume hiyo inaweza kujiuzuru muda wowote