Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa mtu yeyote anayehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita jela, anapoteza sifa za kuwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa wapiga kura wanaostahili kushiriki katika chaguzi wanakidhi vigezo vya kisheria na maadili ya uraia.