Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi wametangaza matokeo au wananchi wanajua matokeo 2020 kwenye Uchaguzi Mkuu?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Tume ya uchaguzi haiajawahi kuwa kimya kwenye maboresho ya daftari la wapiga kura Kama ilivyo awamu hii, hakuna sehemu unaona Kama wapo kazini. Hali imetulia sana Kama vile hakuna watendaji wa tume au tume may be inakosa resources. Lakini baadhi ya watu wanadai hata vifaa vya uandikishaji wapiga kura vimetoka NIDA ambapo pia kuna uandikishaji unaendelea. Ni Kama vile tume imelala kwa kujua labda hatuna uchaguzi.

Kwa wananchi, lipo kundi kubwa sana la vijana waliofikisha 18 Kati ya 2014 na 2020 lakini kundi ilo alionekani kwenye foleni za kutafuta kadi za kura. Kuna tatizo gani? Au kauli za viongozi wa kisiasa ambazo hazikuwahi kukemewa na tume ya uchaguzi zinachangia kuwakatisha tamaa wananchi? Hata wakina Mama waliokuwa mstari wa mbele kutafuta vitambulisho uwaoni kwenye foleni. Tusipuuzie na kusherekea Bali tujiulize wananchi wanaona uchaguzi haupo Tanzania au wanaona uchaguzi si Bora Tena kwao?

Vyombo vya habari navyo vipo kimya kwenye ili, hawana matangazo wala uhamasishaji, kwanini? Tume imeshindaje kuwa na fedha za kuelimisha wananchi?

Najua watu wana national Id na hivyo wanaamini hakuna umuhimu wa kadi ya kura, kwanini taifa limeshindwa kutofautisha umuhimu wa hizi kadi mbili.

Wapinzani nao wamekaa kimya like Kuna mgomo, mgomo unat
 
Halafu mwisho wa siku wanalalamuka wameibiwa kura wakati hata hawakujiandikisha , Mbowe na Zitto wasicheze na akili za watanzania
 
Kwa maoni yangu naona jambo hili liko hivi, kipindi cha nyuma vitambulisho vya kupigia kura vilikuwa ni official Id yani kila sehemu lazima utaulizwa kitambulisho cha kura. Kwa sasa kuna kitambulisho cha Taifa hivyo watu hawaoni tena umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha kupiga kura. RAI yangu elimu zaidi inatakiwa kutolewa, matangazo ya tume yaongezwe, vyama vya siasa vihamasishe wanachama wao kujiandikisha, mashirika yasiyo ya kiserikali yatoe mafunzo ya uhamasishaji.
 
Tume ya uchaguzi haiajawahi kuwa kimya kwenye maboresho ya daftari la wapiga kura Kama ilivyo awamu hii, hakuna sehemu unaona Kama wapo kazini. Hali imetulia sana Kama vile hakuna watendaji wa tume au tume may be inakosa resources. Lakini baadhi ya watu wanadai hata vifaa vya uandikishaji wapiga kura vimetoka NIDA ambapo pia kuna uandikishaji unaendelea. Ni Kama vile tume imelala kwa kujua labda hatuna uchaguzi.

Kwa wananchi, lipo kundi kubwa sana la vijana waliofikisha 18 Kati ya 2014 na 2020 lakini kundi ilo alionekani kwenye foleni za kutafuta kadi za kura. Kuna tatizo gani? Au kauli za viongozi wa kisiasa ambazo hazikuwahi kukemewa na tume ya uchaguzi zinachangia kuwakatisha tamaa wananchi? Hata wakina Mama waliokuwa mstari wa mbele kutafuta vitambulisho uwaoni kwenye foleni. Tusipuuzie na kusherekea Bali tujiulize wananchi wanaona uchaguzi haupo Tanzania au wanaona uchaguzi si Bora Tena kwao?

Vyombo vya habari navyo vipo kimya kwenye ili, hawana matangazo wala uhamasishaji, kwanini? Tume imeshindaje kuwa na fedha za kuelimisha wananchi?

Najua watu wana national Id na hivyo wanaamini hakuna umuhimu wa kadi ya kura, kwanini taifa limeshindwa kutofautisha umuhimu wa hizi kadi mbili.

Wapinzani nao wamekaa kimya like Kuna mgomo, mgomo unat
Huko nyuma watu walihitaji hivyo vitambulisho vya kura kwa matumizi mengine kama kusajili laini ya simu, kufungua akaunti benki, kumdhamini mtu polisi, kuombea pass ya kusafiria nk. matumizi hayo yamechukuliwa na Kitambulisho cha Taifa.

Vitambulisho vya NIDA vingetolewa kwa urahisi ili vitumike pia kwenye kupiga kura hasa ya URAISI. Udiwani na Ubunge pangekuwepo daftari la makazi kwa ajili hiyo
 
The bottom line ni kwamba we are a nation of cheaters, Premeditated results of election. Watanzania siyo kwamba hawaoni umuhimu wa kujiandikisha au kupiga kura bali wanaliona zoezi la upigaji kura ni MAIGIZO!!. Unawezaje kumshawishi mtu aende kujiandikisha wakati ni juzi juzi tu watu wamepora haki ya watu wakashinda kwa 99.99%? msiwafanye watanzania ni wajinga. Watu wamevunjika sana moyo, huu moyo unarudi vipi? ni kazi ngumu, ni mpaka pale watanzania wataamini kwamba wakipiga kura kura yao ita-count. Tusisahau yaliyotokea kwanye chaguzi za marudio ya ubunge, sehemu kama Kinondoni fujo za wazi na za kitoto zilizosababisha mtoto wa watu kuuwawa zilivunja watu sana moyo.

Serikali ya sasa NIA YAKE YA DHATI inataka kurudisha nchi kuwa ya chama kimoja na hilo wananchi wameliona wanaona hakuna haja ya kujisumbua acha tuongozwe kwa mabavu at least for the time being.

Nini cha kufanya? Tufanye mjadala wa kitaifa tutafute ni namna gani tutatendeana haki kwenye zoezi la kutafuta viongozi. Siyo tu kuahidi utatenda haki bali vitendo vionyeshe kwamba mpiga kura atatendewa haki. Kwa mfano mwananchi akifikiri kwamba anayesimamia uchaguzi - mkurugenzi ni mteuliwa wa rais na ni kada wa chama tawala ni vigumu kumuaminisha kwamba atatenda haki. Mwananchi lazima aaminishwe kwamba huyu msimamizi ni neutral and impartial. Mwananchi anaona mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ni mteuliwa wa rais hawezi kuamini asilimia 100. Kama tuna nia ya dhati kabisa ya wanachi kujichagulia viongozi tubadili mfumo wa kuwapata wasimamizi. Baada ya kufanya hayo ifanywe kampeni mahsusi ikivishirikisha vyama vyote vya siasa na vyombo vya habari kuwatangazia wanachi kwamba mfumo wetu wa uchaguzi kwa sasa utakuwa wa haki.

Mbona tulikuwa tunapiga kura wakati wa chama kimoja? ni kwamba haki ilikuwa inatendeka, nakumbuka pale miaka ya themanini pale Bukoba mjini kampeni za ubunge zilikuwa motomoto sana kati ya Luangisa na Katalaiya watu walihamasika kwa kuwa waliamini moja itakuwa moja na mbili itakuwa mbili. Sasa hivi moja inaweza kuwa 10!!!
 
Wengi hawana mwamko wa kujiandikisha, matendo ya kidhalimu yanayofanywa wakati wa kupiga kura yamewachosha wengi, watu wanaona wazi wazi kura zao zikiibwa, wagombea wa upinzani kukamatwa wakati zoezi la upigaji kura likiendelea (Kinondoni) halafu wanaachiwa baada ya wananchi kumaliza kupiga kura, mawakala wa upinzani kuzuiwa kuingia vituoni kufuatilia zoezi la upigaji kura likiendelea, wakati mwingine mawakala/wagombea wa upinzani wanatekwa, kupigwa, na kuumizwa.

Ni nani atakuwa na hamu ya kupiga kura kwenye mazingira hayo? yaliyojaa uonevu, wizi, dhuluma, za waziwazi.

Ndio maana wengi sasa wameamua kukimbilia CCM kwasababu wanapaona ndio sehemu salama zaidi kwao, ukiwa huko huna haja ya kuamini kwenye nguvu ya wapiga kura, wanajua watapewa ushindi kwa kutumia jeshi la polisi. Kuwa mpinzani Tanzania awamu hii ni sawa na ku-sign hati ya kifo, unakisubiri dakika yoyote, but kuna wajinga wengi tu wanashangilia yote haya, wakiaminisha umma CCM inakubalika! ni watu jasiri pekee watakaobaki upinzani, but legelege wote lazima wakimbie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tume ya uchaguzi haiajawahi kuwa kimya kwenye maboresho ya daftari la wapiga kura Kama ilivyo awamu hii, hakuna sehemu unaona Kama wapo kazini. Hali imetulia sana Kama vile hakuna watendaji wa tume au tume may be inakosa resources. Lakini baadhi ya watu wanadai hata vifaa vya uandikishaji wapiga kura vimetoka NIDA ambapo pia kuna uandikishaji unaendelea. Ni Kama vile tume imelala kwa kujua labda hatuna uchaguzi.

Kwa wananchi, lipo kundi kubwa sana la vijana waliofikisha 18 Kati ya 2014 na 2020 lakini kundi ilo alionekani kwenye foleni za kutafuta kadi za kura. Kuna tatizo gani? Au kauli za viongozi wa kisiasa ambazo hazikuwahi kukemewa na tume ya uchaguzi zinachangia kuwakatisha tamaa wananchi? Hata wakina Mama waliokuwa mstari wa mbele kutafuta vitambulisho uwaoni kwenye foleni. Tusipuuzie na kusherekea Bali tujiulize wananchi wanaona uchaguzi haupo Tanzania au wanaona uchaguzi si Bora Tena kwao?

Vyombo vya habari navyo vipo kimya kwenye ili, hawana matangazo wala uhamasishaji, kwanini? Tume imeshindaje kuwa na fedha za kuelimisha wananchi?

Najua watu wana national Id na hivyo wanaamini hakuna umuhimu wa kadi ya kura, kwanini taifa limeshindwa kutofautisha umuhimu wa hizi kadi mbili.

Wapinzani nao wamekaa kimya like Kuna mgomo, mgomo unat

Wananchi wameamua kumuonyesha Magufuli na chama chake kuwa hawawataki wala kuwakubali. Na kwakuwa wanajua tume ya uchaguzi haiko huru hawako tayari kupoteza muda kwenye kura zisizoheshimiwa. Watatafuta njia nyingine ya kupata viongozi nje ya huu utaratibu rasmi.
 
Wengi hawana mwamko wa kujiandikisha, matendo ya kidhalimu yanayofanywa wakati wa kupiga kura yamewachosha wengi, watu wanaona wazi wazi kura zao zikiibwa, wagombea wa upinzani kukamatwa wakati zoezi la upigaji kura likiendelea (Kinondoni) halafu wanaachiwa baada ya wananchi kumaliza kupiga kura, mawakala wa upinzani kuzuiwa kuingia vituoni kufuatilia zoezi la upigaji kura likiendelea, wakati mwingine mawakala/wagombea wa upinzani wanatekwa, kupigwa, na kuumizwa.

Ni nani atakuwa na hamu ya kupiga kura kwenye mazingira hayo? yaliyojaa uonevu, wizi, dhuluma, za waziwazi.

Ndio maana wengi sasa wameamua kukimbilia CCM kwasababu wanapaona ndio sehemu salama zaidi kwao, ukiwa huko huna haja ya kuamini kwenye nguvu ya wapiga kura, wanajua watapewa ushindi kwa kutumia jeshi la polisi. Kuwa mpinzani Tanzania awamu hii ni sawa na ku-sign hati ya kifo, unakisubiri dakika yoyote, but kuna wajinga wengi tu wanashangilia yote haya, wakiaminisha umma CCM inakubalika! ni watu jasiri pekee watakaobaki upinzani, but legelege wote lazima wakimbie.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwenye red hapo umesema ukweli na hii ni aibu kwa jeshi, ndo maana mtu muadilifu kama Sirro alitaka kujiuzulu kwa kuwa maadili ya kazi yake yanavunjwa kwa shinikizo
 
Halafu mwisho wa siku wanalalamuka wameibiwa kura wakati hata hawakujiandikisha , Mbowe na Zitto wasicheze na akili za watanzania
Heeeh!! Karlo Mwilapwa, vp tena inamaana Mbowe na Zitto ndo wanaandikisha au wanawakataza watu kujiandikisha? tufafanulie ndg yang ili tuchukua hatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matokeo yalishatangazwa tayari Magufuli ameshinda kwa asilimia 99.9 kinachofuata nikubalikiwa kwa uchaguzi fake utakaotangazwa na tume huru fake toka CCM.
 
Back
Top Bottom