The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Tume ya Uchaguzi ya Namibia (ECN) imeeleza wasiwasi wake kuhusu idadi ndogo ya watu wanaojiandikisha kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi ujao ikiwa zimebaki wiki mbili tu.
Hayo yamesemwa na afisa mkuu wa uchaguzi wa ECN Peter Shaama katika mkutano na waandishi wa habari.
Bwana Shaama amesema: “Ingawa tunakubali kuwa kumekuwa na ongezeko kidogo la idadi ya waliojitokeza kati ya wiki ya tarehe 1 hadi 6 Julai ikilinganishwa na wiki ya tarehe 24 hadi 29 Juni, tume bado inaona kwa wasiwasi idadi ndogo ya waliojitokeza nchi nzima hadi sasa,”
“Tume inawahimiza raia wote wa Namibia wanaostahili kupiga kura ambao bado hawajajisajili kufanya hivyo ndani ya wiki zilizobaki,” alisema.
Shaama alisema hakuna nafasi ya kuongeza muda wa kujiandikisha kupiga kura.
Usajili utaendelea nchi nzima na katika ofisi zote za kidiplomasia za Namibia nje ya nchi hadi tarehe 1 Agosti, Jumatatu hadi Jumamosi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 1:00 usiku.
The Namibian