Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yatangaza Uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura

Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yatangaza Uwekaji wazi wa daftari la awali la wapiga kura

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura kwa siku 4 kuanzia Juni 17 mpaka Juni 20 katika vituo vilivyotumika wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kwa ajili ya uhakiki

Afisa kutoka Idara ya Elimu ya Mpiga Kura, Salma Said Mohammed amesema katika zoezi hilo vituo vyote vitafunguliwa saa 2 kamili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni kwa siku zote 4

Amesema NEC inaweka wazi Daftari hilo kwa lengo la kutoa fursa kwa Wapiga Kura kuweza kuhakiki taarifa zao na kufanya marekebisho ya taarifa ikiwa taarifa hizo zimekosewa

Mpiga Kura anaweza kwenda kwenye kituo kilichopangwa na Tume au anaweza kutumia huduma ya ujumbe mfupi kupitia mitandao yote ya simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# au kupiga moja kwa moja kituo cha huduma kwa mpiga kura kupitia na 0800112100 na kufuata maelekezo baada ya kupiga namba hizo

Aidha, mpiga Kura anaweza kuhakiki taarifa zake kupitia tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ni www.nec.go.tz na kubonyeza sehemu ya kuhakiki na kufuata maelekezo.

1592220978537.png

1592220991823.png
 
Back
Top Bottom