PostGE2025 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yateketeza nyaraka za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imeanza utekelezaji wa zoezi la kuteketeza nyaraka za Uchaguzi Mkuu uliofanyia Oktoba 29, 2025 ambapo zoezi hilo limeanzia Kisiwa cha Pemba na baadae Kisiwa cha Unguja.

​
Akizungumza kuhusu zoezi hilo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jaji George Joseph Kazi amesema uteketezaji wa nyaraka hizo ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria kwa mujibu wa Kifungu cha 98(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar ya mwaka 2018 ambayo inaipa Tume mamlaka ya kuteketeza nyaraka za Uchaguzi baada ya siku 90 tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu endapo hakuna katazo kutoka Mahakamani.

Aidha Jaji George Kazi ameeleza kuwa anatambua ya kuwa kuna kesi ambazo zinaendelea Mahakamani kuhusu Uchaguzi Mkuu uliyofanyika Oktoba 2025 lakini mpaka kufikia siku ya jana hawajapokea katazo lolote kutoka Mahakamani hivyo Tume imeteketeza nyaraka hizo kwa mujibu wa Mamlaka iliyopewa kisheria.

Your browser is not able to display this video.
 
wako sahihi kwa mujibu wa sheria na katiba ya SMZ
 
ACT Wazalendo mna kesi kudai wabunge wenu wameshinda 2025 Huku ZEC wanachoma kura na nyaraka mlizoshindwa kulinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…