Ni kweli kwamba mwaka 2010 matokeo ya kidato cha Nne hayakuwa mazuri hali iliyopelekea serikali kuunda tume ili kutafuta chanzo na sababu za hali hiyo. Tunapenda watanzania wapewe matokeo ya uchunguzi wa tume hiyo kabla ya kupoteza fedha za walipa kodi kwa kuunda tume nyingine kwa ajili ya suala lile lile.