DOKEZO Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ishughulikie wanaosambaza taarifa zetu kiholela

DOKEZO Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ishughulikie wanaosambaza taarifa zetu kiholela

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Kwa masikitiko makubwa ni fedhea kwa kampuni inayojishughulisha na uuzaji wa Virutubisho (Supplements) na bidhaa za usafi kama NeoLife kushindwa kuhifadhi Tarifa binafsi za wateja wake kama inavyotakiwa .

IMG_4325.png



Asubuhi nimenunua vitumbua maeneo ya Mwenge kituoni na kifungashio kilichotumika kilikuwa ni fomu ya kampuni ya NeoLife ikiwa na tarifa binafsi za mmoja wa wateja wao.

Licha ya fomu hiyo kuandikwa herufi kubwa "Private and Confidential" lakini bado fomu hiyo ilikuwa inazagaa mitaani kama vifungashio vya vitumbua.

Fomu hiyoo ilikuwa na majina kamili ya mteja, tarehe yake ya kuzaliwa, aina ya dawa alizonunua, kiasi na lilipia shilingi ngapi pamoja na namba za simu.

Sasa najiuliza tarifa binafsi kama hizi zidondokea mikono mwa mikono ya wahuni si wanaweza kutumia hizi taarifa za huyu mtu vibaya jamani.

Taarifa hizi zinaweza kutumika kufanya uwizi na shughuli nyingine za kihalifu na hata mtu wingine anaweza kuiba utambulisho wa huyu mteja na kufanya uhalifu.

Basi mmengeficha au kufuta baadhi ya taarifa zake. Mnapaswa kuchukua hatua sahihi za kuteketeza taaarifa za wateja wenu badala ya kuuza haya makaratasi kama vifungashio.

Soma Pia: Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) itusaidie kushughulikia wanaosambaza taarifa zetu kiholela. Vyeti vyetu vinafungiwa kachori

Kwa mwenendo huu Kamati ya Tarifa Binafsi ni wakati wa kuchukua hatua taasisi zinzovujisha taarifa binafsi zinazovujisha taarifa binafsi za watu na pia kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu suala hili
 
Unanunua KITUMBUA halafu unataka kufichiwa siri ..!!

Acha kununua vitumbua vyao!

Coz yaonekana muuza vitumbua ni staff wao


KATOA WAPI FORM SENSITIVE HIVYO
 
Wangechoma tu hayo makaratasi kama yalikwisha expire
 
Hio si Order form? Anakua nayo mteja mwenyewe(kumbuka wateja wake wa direct ni wanachama) akitaka kuagiza bidhaa, anajaza halafu anapiga picha anatuma..
Nijuavyo lakini.
 
Back
Top Bottom