KERO Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) itusaidie kushughulikia wanaosambaza taarifa zetu kiholela. Vyeti vyetu vinafungiwa kachori

KERO Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) itusaidie kushughulikia wanaosambaza taarifa zetu kiholela. Vyeti vyetu vinafungiwa kachori

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Hapa chini ni nyaraka zenye taarifa binafsi za mtu ambaye anaonekana aliomba nafasi ya kazi mahali fulani, lakini baada ya nyaraka zake kuisha kuisha umuhimu wakazitelekeza kiholela. Sijui waliuza hizo karatasi au walitupa watu wakaokota, haieleweki. Ila sasa zinapatikana kwa akina mama wauza vitumbua.

Jambo hili sijui lizungumzwe mara ngapi! Taasisi nyingi bado zinafeli sana katika suala la kuhifadhi au kuteketeza nyaraka ambazo zina taarifa binafsi za watu kwa njia inayofaa. Badala yake, wanazitupa nyaraka hizo kiholela au bila ya kuchukua tahadhari, hali inayoweza kusababisha taarifa hizo kuangukia mikononi mwa watu wasiostahili.

Hii inaweza kuwa na madhara makubwa sana, sana kwa faragha na usalama wa watu, kwani taarifa binafsi kama vile majina, namba za simu, anuani, matokeo ya shule, taarifa za vitambulisho vya taifa, au taarifa za kifedha n.k zinaweza kutumiwa vibaya na wahalifu au watu wenye nia mbaya.

Soma Pia:
Ifike mahali sasa kila taasisi kuwa na utaratibu madhubuti wa kuteketeza nyaraka ili kulinda taarifa za watu na kuhakikisha kuwa hazitumiwi kinyume cha sheria au kwa madhumuni yasiyofaa. Kwa mfano kuna zile mashine zinaitwa paper shredder, kwanini isiwe ni kifaa cha lazima kila ofisi inayochakata nyaraka za karatasi kumiliki na kusimamia uteketezaji wa nyaraka hizo?

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) mmelifungia hili vioo? Ingawa taarifa nyingi zinahamia mtandaoni, lakini bado kuna haja ya kushughulikia vema hawa wanaotusambazia taarifa zetu mtaani kiholela. Onesheni mfano kwa taasisi kadhaa wengine wajifunze.

zu1.jpg
zu3.jpg

zu 2.jpg
 
Hizo nyaraka uwa ni dili kwa watumishi wa kitengo cha utunzaji wa nyaraka na walinzi wa taasisi. Kwa wingi wake uwa wanapata marundo na kuwauzia watu wanaoshughulika na utengenezaji wa vifungashio kama hivyo.
 
Kiukwel taarifa binafsi kama hizo zinatakiwa Kuwa sehemu salama Ili kuhakikisha wale wasio husika nazo wasiweze kuzipata Ili kuepukana na changamoto zinazoweza kujitokeza.
 
Back
Top Bottom