JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Dkt. Noe Nnko
Akizungumza Machi 1, 2025, wakati wa kuwasilisha mada kuhusu teknolojia za ulinzi wa taarifa, changamoto zake, na umuhimu wa kuwa na sera za kusimamia taarifa binafsi kwa wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Mkurugenzi wa Tafiti za Ulinzi wa Taarifa na Teknolojia, Dk. Noe Nnko, amesema taasisi zote zinapaswa kuwa na afisa maalum wa kusimamia taarifa binafsi.
"Taasisi zinapaswa kuwa na afisa wa taarifa binafsi aliyefundishwa kutunza taarifa za watu kwa usahihi. Hata tarehe ya kuzaliwa ya mtu ni taarifa binafsi ambayo hairuhusiwi kutumiwa bila idhini," amesema Dk. Nnko.
Aidha, alisisitiza kuwa mtu ana haki ya kuomba taarifa zake ziondolewe kwenye tovuti, mitandao ya kijamii, au majukwaa mengine ikiwa zinatumika kinyume cha sheria.
Chanzo: Nipashe
Pia soma:
~ Ijue Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, sheria no. 11 ya mwaka 2022
~ Ma-MC wanaosambaza picha za Watu bila ridhaa waonywa
~ PDPC: Ukifika nyumba ya Kulala Wageni, marufuku kuandika unapotoka na unapokwenda