Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaonya ufungaji wa Kamera (CCTV) kwenye maeneo ya faragha

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaonya ufungaji wa Kamera (CCTV) kwenye maeneo ya faragha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
photo_2024-06-24_18-40-40.jpg

YAH: ONYO DHIDI YA KUFUNGA VIFAA VYA USALAMA (CCTV) KWENYE MAENEO YA FARAGHA

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi - PDPC inatoa onyo kali kwa Taasisi na kampuni zote zinazotumia kamera za usalama ikiwa ni pamoja na maeneo ya kazi kuhakikisha wanazingatia Sheria na Kanuni za Ulinzi wa Taarifa Binafsi Tanzania.

Kumekuwa na taarifa za uwepo wa matukio ya kuwekwa kamera za usalama (CCTV) katika maeneo ya faragha, kama vile vyooni, ambapo ni uvunjaji wa haki ya faragha na ni kinyume na sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.

Taasisi na kampuni zote nchini zinakumbushwa kuzingatia kikamilifu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11,2022 na Kanuni zake wakati wa kufunga mifumo ya usalama maeneo ya kazi au nyumbani. Ni muhimu hatua zozote za ufuatiliaji ziwe za uwiano na zenye kuheshimu haki za faragha za watu.

Tunatoa wito kwa wadau wote kufanya mapitio ya kina ya vitendo vyao vya ufuatiliaji na kuhakikisha kuwa wanazingatia kikamilifu Sheria na Kanuni za Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Heshima kwa faragha ya mhusika wa taarifa ni ya msingi, na ni jukumu la kila Taasisi kulinda Taarifa Binafsi za watu.

Kwa mwongozo na taarifa zaidi kuhusu Ulinzi wa Taarifa Binafsi, tafadhali wasiliana nasi kupitia mitandao yetu ya kijamii au tupigie kwa namba zetu za huduma kwa wateja.

Imetolewa leo Jumatatu Juni 24, 2024 na:

Mkurugenzi Mkuu,
Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
"FARAGHA YAKO NI WAJIBU WETU"

Pia soma
~ Naomba uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili uondoe CCTV Camera zilizowekwa chooni
~ Hospitali yaTaifa ya Muhimbili kweli mmeamua kutuvua nguo kwa kufunga camera kwenye vyoo, hamjui mnaingilia faragha zetu?
 
Back
Top Bottom