Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yazionya Taasisi za mikopo zinazodhalilisha watu ikiwemo kutuma ujumbe kwa ndugu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Emmanuel Mkilia amezionya Taasisi na Watu Binafsi wanaotoa Mikopo na kisha kuwadhalilisha Wakopaji ikiwa wameshindwa kurudisha Mikopo

Amesema, “Tutoe onyo kwa watu/Taasisi za Mikopo zinazowanyima haki ya faragha wateja kwa kuweka mikataba mibovu ya mikopo ambayo mteja asipoweza kulipa kwa wakati jumbe za kudhalilisha utu wake zinatumwa kwa watu wake wa karibu. Waache mara moja”

Pia soma;
1. Taasisi zinazotoa mikopo zitunze faragha za wateja wao

2. DOKEZO - Taarifa Binafsi zinakusanywa na "Kampuni za Mikopo Mtandaoni" ni Hatarishi kwa Faragha ya Mtu

3. KERO - Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

4. KERO - Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Iwashughulikie Wakopeshaji wa Mtandaoni Wanaodhalilisha Wateja Wao Kwa Kusambaza Taarifa Binafsi Kwa Wasiohusika

5. Nape: Tumewaagiza TCRA wachunguze wale wanaodhalilisha watu waliowakopesha Mtandaoni
 
Aise bora maana nikero sana mtu anakuzamini ww ujui unajikita unapigiwa simu na kutishiwa unatafutwa kwa kosa la kumzamini mtu pesa ambayo hata hujui
 
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Emmanuel Mkilia amezionya Taasisi na Watu Binafsi wanaotoa Mikopo na kisha kuwadhalilisha Wakopaji ikiwa wameshindwa kurudisha Mikopo

Amesema, “Tutoe onyo kwa watu/Taasisi za Mikopo zinazowanyima haki ya faragha wateja kwa kuweka mikataba mibovu ya mikopo ambayo mteja asipoweza kulipa kwa wakati jumbe za kudhalilisha utu wake zinatumwa kwa watu wake wa karibu. Waache mara moja”
Hili Agizo ni kama limechelewa. Kwani Mkurugenzi alipopitisha Kibali cha hizo Taasisi na Watu Binafsi hakukagua na kusoma kwa undani Memorandum of Understanding (MoU) walizowasilisha kwake kuomba kibali? au ilikuwaje.... halafu sasa watu wengi wameshaumizwa ndipo anazinduka?
 
Yeye kwa nafasi yake amefanya kazi gani kukomesha jambo hilo au anakula mishahara bure tu, kwanini ameliacha hadi kuwa donda ndugu
 
@branch mmeona hii habari.
Kuanzia Leo msinipigie simu zenu. Sikuwalazimisha kunikopesha, after all shilingi laki tatu Ni kitu gani?
 
Yan mwamba hapo umebugi sana katika makampuni ambayo hayana shida bas ni branch kwa mda wakulipa unachagua mwenyewe tena mwezi mmoja hadi miwili tena riba yao ndogo sana alafu hawana Mambo mengi sijui yakupiga picha sijui ya kitambulisho wala nini
 
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Emmanuel Mkilia amezionya Taasisi na Watu Binafsi wanaotoa Mikopo na kisha kuwadhalilisha Wakopaji ikiwa wameshindwa kurudisha Mikopo

Amesema, “Tutoe onyo kwa watu/Taasisi za Mikopo zinazowanyima haki ya faragha wateja kwa kuweka mikataba mibovu ya mikopo ambayo mteja asipoweza kulipa kwa wakati jumbe za kudhalilisha utu wake zinatumwa kwa watu wake wa karibu. Waache mara moja”

Pia soma;
1. Taasisi zinazotoa mikopo zitunze faragha za wateja wao

2. DOKEZO - Taarifa Binafsi zinakusanywa na "Kampuni za Mikopo Mtandaoni" ni Hatarishi kwa Faragha ya Mtu

View: https://youtu.be/JilJhn_tP-c
👆 👆 Haya mambo yameshafanyika hadi India sis ndio tunaamka leo
 
Mimi mwenyewe ni muhanga wa Hilo nilikopa kwenye moja ya wakopeshaji online nilikua nashida ya haraka sana nilikua shamba kuna rafiki yangu akaniambia kopa online nichap mpkaa mtu upate mtu wakukukopesha haraka muda unaenda nikakopa Sasa nikachelewa kulipa ndani ya zile siku sita kwasababu nilikua shamba na hata nilipowaambia mahali nilipo nichangamoto kupata wakala kwa haraka walikataa ilipofika saa 2 usiku mtu wakwanza kunipigia nibosi wangu kazini nanilionekana mm tapeli watu wote ambao namba zako zipo kwenye simu yangu walitumiwa meseji na ushahidi meseji nihii.
HABARI NDUGU AMA JAMAA WAKARIBU WA YUSUPH SHABAN MBWAMBO MWENYE UMRI WA MIAKA 34 NO; 0677xxxxxx AMEKOPA KIASI CHA SHILLINGI 56,700/= KUTOKA KAMPUNI YA MY CREDIT ANATAKA KUTUTAPELI, UKIWA KAMA MTU WAKE WA KARIBU TUNAOMBA UMUAMBIE ALIPE DENI LAKE KABLA HATUJAANZA KUCHUKUA HATUA NYINGINE JUU YAKE.
 
Mi silipi, deni sio dhambi, kama nilishadhalilika nililelewa ukweni nikakojoa hadharani tena mbele ya kadmnasi iliyokuwa msibani, nishakamatwa na wakwe napiga nyeto, kuna aibu gani nyingine, kwanza contact list yangu wote wananijua kwa madeni hamna aibu mpya, sahivi nakopa kwa vitambulisho vingine maana cha kwangu wamekipiga ban
 
Hakuna eneo wananchi wanapigwa kama hili, mobile loan ni tatizo kubwa Tanzania na halina weledi kabisa .. Imagine mtu anakopewa pesa kiduchu riba lundo ! Wakopaji wanafedheheshwa, wanazalilishwa, wananyanyasika .. Serikali ikomeshe huu wizi, sauti zaidi zipazwe. USTAWI LOANS Mr. Finance wanaongoza kuzalilisha watanzania kupitia hii mikopo haramu.
 
Hawa wanatakowa wakamatwe haraka
 
Serikali ikomeshe hiki kikundi haraka
 
Back
Top Bottom