DOKEZO Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC) na Utumishi wa Umma ngazi ya taifa watoe mwongozo kuhusu kero za walimu kubadilisha miundo (recategorization)

DOKEZO Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC) na Utumishi wa Umma ngazi ya taifa watoe mwongozo kuhusu kero za walimu kubadilisha miundo (recategorization)

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wilaya ya Bunda maafisa utumishi na TSC wanawasumbua walimu waliojiendeleza na kuwa na sifa ya kubadili miundo yao katika ajira kama kutoka daraja la IIIA au IIIB kwenda IIIC.

Mtumishi anafualitilia hilo jambo miaka mingi na halishughulikiwi kwa muda badala yake wanatoa majibu ya "njoo kesho, njoo mwezi January, ikama hairuhusu, muda wa kufanya recategorization umeisha subiri mwaka wa fedha ujao" walimu ni wavumilivu wanasubiri, muda ukifika wanaanza kupigwa kalenda zilezile ikiwemo kupoteza barua za mtumishi aliyeomba kwa utaratibu na mtumishi huyo atatakiwa kuanza tena upya ombi lake.

Pia wanatoa majibu ya kukatisha tamaa, wakisema "kwa mujibu wa sheria hata ukibadilisha muundo hautabadilishiwa mshahara na hautoongezeka" na hawasemi ni sheria ipi?

Sasa tunaona kwenye halmashauri nyingine watumishi wakibadilishwa miundo yao na mshahara hulipwa kulingana na muundo husika.

Hii si sawa kabisa, na hali hii inatengeneza mazingira ya rushwa pia inavunja moyo wa kufanya kazi kwakuwa watumishi huwa wanasisitizwa kujiendeleza, lakini baada ya kujiendeleza ni kama wanakuwa maadui kwa viongozi.
 
Back
Top Bottom