DOKEZO Tume ya Utumishi Zanzibar inaita waajiriwa wapya kimya kimya. Itoe orodha kamili ili kuziba mianya ya rushwa na upendeleo

DOKEZO Tume ya Utumishi Zanzibar inaita waajiriwa wapya kimya kimya. Itoe orodha kamili ili kuziba mianya ya rushwa na upendeleo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hivi karibuni kumekuwa na usaili wa ajira mbalimbali ambao umefanyika na unaendela kufanyika Pemba na Zanzibar.

Kwa upande wa ajira za Ualimu kwa mfano Ilitoka list ya walioitwa Interview ya kwanza ya maandishi (written interview) na haikuzidi siku tatu list ya Interview ya pili ya ana kwa ana (Oral interview) imetoka. Lakini cha kushangaza ni zaidi ya wiki ya tatu hii, hayajatoka matokeo ya Placement (Yaani wanaoitwa kazini).

Cha kushangaza zaidi ni kuwa watu wanaoitwa kazini huitwa kimya kimya, hali inayopelekea wenye mamlaka kuweka watu wao tofauti na waliofanya interview ama kwa kutoa rushwa au kujuana, hata kuuza nafasi jambo ambalo limekuwa ni kero kubwa na linaleta wasi wasi kwa raia.

Tunaomba wahusika wawajibike kwa hili na wajitahidi kuiga wenzao wa Tanzania bara ambapo hawazidi siku tatu kwa matokeo ya kila interview. Lakini pia watoe na list ya Placement yaani majina au no za interview za walioajiriwa ili kuziba mianya, kuleta usawa na kuondoa ukakasi kwa raia wote.
 
Back
Top Bottom