Tume ya warioba zanzibar

Tume ya warioba zanzibar

abdul 28

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2012
Posts
325
Reaction score
38
Tarehe 19 December ilikuwa siku ya mwisho kwa Tume ya Kukusanya maoni ya upatikanaji wa katiba mpya. Tume ilifanikiwa kutemebelea nchi nzima na kukutana na wananchi walioweza kutoa dukuduku lao na vipi katiba mpya itapatikana. Kwa mujibu wa hadidu rejea za tume hityo zilizotolewa ni kwamba baada ya kumaliza kazi ya ukusanyaji maoni kwa wananchi kutakuwa na mabaraza ya katiba.

Hivi sasa hapa Zanzibar kuna taarifa za kuaminika kwamba baadhi ya wizara zimetowa toleo maalim (circular) la kuwataka wafanyakazi wa serikali watowe maoni yao ya kwa njia za maandishi. Toleo limepelekwa idara mabalimbali za serikali kuwataka wafanyakazi waandike maaoni yao juu ya mchakato wa katiba. Hili ni lakushangaza kwamba waliotoa toleo hili sio Tume ya Katiba wala halimo kwenye hadidu rejea za Tume hiyo. Hivyo kutia wasiwasi muelekeo wa upatikanaji wa katiba mpya Tanzania kugubikwa na magube ya kimapinduzi.

Zipo dalili za dhahiri za kukengeukwa na kudharauliwa maoni ya wananchi kama vile walivyotumia juhudi zao, wakavunja shughuli zao, wakatumia muda wao, na mwisho kile walichosema kuanza kukidharau. kauli ya Prof baregu ni ushahidi tosha na mwanzo wa kuthibisha hili. Dharau yake kwa maoni ya wananchi hasa Wazanzibar, sio suala la kuvumiliwa. Ipo haja kwa nguvu zote tuisute tume pale itakapozidisha dharau zake kutothamini maoni ya wananchi.
 
..mbona naona kama tume imetumia muda mrefu sana kuchukua maoni ya wa-ZNZ.

..it's about time wa-concentrate na huku Tanganyika ukizingatia kwamba sisi ndiyo tunabeba mzigo wa gharama za tume hiyo.
 
..mbona naona kama tume imetumia muda mrefu sana kuchukua maoni ya wa-ZNZ.

..it's about time wa-concentrate na huku Tanganyika ukizingatia kwamba sisi ndiyo tunabeba mzigo wa gharama za tume hiyo.
Ndio ujue kuwa ZNZ ni muhimu kwenye huo mchakato. 'Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi'
 
kuhusu muungano sisi wenyewe watanzania hatujui muungsno wetu ukovipi,itakuwaje akiulizwa mtu wa Kenya,lamuhimu ni kuuvuja kwanza.
 
Ndio ujue kuwa ZNZ ni muhimu kwenye huo mchakato. 'Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi'
Freshthinking,

..kama ni hivyo basi ZNZ wachangie gharama za matumizi ya tume hiyo.

..wao walikuwa mstari wa mbele kudai wajumbe wao nusu kwa nusu, lakini kwenye kuchangia gharama wameuchuna.

..hata muungano wa mkataba mnaopendekeza huenda mnataka kuendeleza unyonyaji tu. ndiyo maana wengine tunataka Tanganyika huru itakayokuwa na mashirikiano na Zanzibar kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki, au SADC.
 
Last edited by a moderator:

Wanachotaka Zanzibar ni nchi yao kamili. Kusema muungano wa mkataba ni lugha ya kiungwana sawa na kusema HATUTAKI MUUNGANO.Hila mbinu mtazifanya nyie watanganyika kwa mfano a kutisha waajiri na waairiwa kutoa maoni mengine ya eti kuunga mkono muungano au upoteze kazi. Yote ya nini haya?

Kwa nini tuligharamikie jambo ambalo hatulitaki? Nyie mnaodhania mtaendelea kututawala kimbavu ndio mnopaswa kunyenyekea na kutukubalie masharti yetu.
ZANZIBZR HURU INAWEZEKANA
 
Back
Top Bottom