Tume ya waziri mkuu na matokeo yenye utata

Papaa Kinyani

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2013
Posts
1,459
Reaction score
699
Mapendekezo kuhusu matokeo tata
Mwenyekiti wa tume ya waziri mkuu ya kuchunguza sababu za kushuka kwa ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2012, amesema kuwa kuna mapendekezo mengi na baadhi ameyatoa. Sasa, ni vizuri tuchunguze sana ripoti hiyo. Inaonekana kuwa ripoti hiyo haina uhalisia kwa Tanzania.

Kusema simu zinaweza kutumika kuhifadhi vitabu, ni kwenda kinyume na kanuni za wizara zinazomkataza mwanafunzi kumiliki simu ya mkononi shuleni. Pia, anapotoa mfano kuwa magazeti kama mwananchi yanaweza kuandika mada za vitabu halafu wanafunzi wanunue magazeti hayo kwa ajili ya kusoma mada zinazofundishwa darasani, ni pendekezo la kufikirika tu. Magazeti yaandike mada za waandishi gani? Je, mhariri wa gazeti anafahamu nini kuhusu hiyo mada? Je, wanafunzi watanunua magazeti mangapi na kuhifadhi wapi? Sio vizuri Prof Sifuni Mchome kutupotezea muda kwa kutoa mawazo dhaifu ya kutudanganya.

Kuhusu mzunguko wa mitaala, mwenyekiti wa tume ametaja mitaala ya aina tatu. Mitaala ya miaka saba kwa shule za msingi, miaka minne kwa kidato cha nne na ya miaka miwili kwa kidato cha sita. Amefafanua kuwa kila mtaala unapomaliza mzunguko wake, mzunguko wa mtaala mpya uanze mara. Hivyo kuwe na mizunguko aina tatu. Mizunguko ya miaka saba, minne na miwili. Kwa hiyo kila mzunguko unapoisha, mtaala mpya wa mzunguko huo uanze mara. Mzunguko wa mtaala ni kipindi ambapo mtaala mpya unaza na wanafunzi wa darasa la kwanza kwa shule za msingi hadi wanamaliza darasa la saba na mtaala huo hufanya mzunguko mmoja.

Mawazo haya sio ya kiutendaji. Kuanza mzunguko mpya kwa kuwa uliopo umekwisha sio sababu hata kidogo. Mzunguko wa mitaala sio sawa na mizunguko ya chaguzi za siasa au marais ambao hutokana na kipindi cha utawala wake kuisha. Lazima ziwepo sababu za kitalaamu pamoja na tafiti ambazo zitaibua kuanza mzunguko mpya. Kwa chombo kama Taasisi ya Elimu kinatakiwa kuwa na utaratibu wa kuanzisha na kumaliza mizunguko ya mitaala.

Pamoja na kuwa kuna mizunguko mitatu, chombo hicho kinaweza kuunda mfumo ambao mitaala yote mitatu inaenda kwa kutumia mzunguko mmoja. Hivyo mzunguko huo uanze muda fulani na kuisha muda fulani. Hii ni kwa ajili ya kurahisisha uendeshaji wake. Cha msingi ni kuwa wakati mzunguko unatekelezwa, wahusika wanachunguza mafanikio na mapungufu katika kila mtaala.

Kwa kufuatilia vitu vinavyoibuka wakati wa utekelezaji wa mitaala katika mzunguko uliokubalika, maamuzi kadhaa yanaweza kufanyika mwishoni wa mzunguko. Maamuzi haya yanaweza kuwa ni kubadili mitaala au kuurekebisha kwa baadhi ya mihtasari na hata kusema iendelee kama ilivyo. Hii ndio hali inayotaka kuwepo na mzunguko wa mitaala.
 
Hao vilaza wameshatafuna pesa na hawana jipya la kuwaambia wananchi. Hivyo ni lazima kubuni tu ya kujazia report.
 
Tume inasema ina mapendekezo 130.Kinachowasukuma kuanza kuweka hadharani mapendekezo nusu nusu tena kwa njia ya kukutana na waandishi wa habari ni nini?Wamesema hiyo kazi ya kuchunguza matokeo ya kidato cha nne 2012 itakamilika mwezi juni wanatakiwa watoe taarifa kamili badala ya kuleta usanii.
 
elimu tata,matokeo tata na hata maelezo ya viongozi husika yana utata!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…