"UTAJIRI unaotokana na wizi wa mali ya umma, na wizi wa fedha za kigeni na unyonyaji na uharamia wa aina mbalimbali, hautupunguzii umaskini wetu, bali unauongeza. Chama chetu hakiwezi kuikubali hali hii, na kikaendelea kuwa CCM, na wala kisitazamie kuwa wananchi wataendelea kukikubali" (Mwalimu Nyerere, Oktoba 1987).
MAFISADI KAZI KWENU WATANZANIA WAMEAMKA NA SASA WANATAKA NCHI YAO. SIKU INAKUJA TUTAWAHUKUMU NA MTAFIA MAGEREZANI MLIKOWEKA WANYONGE MLIOWAIBIA UTAJIRI WAO MKAWALAZIMISHA WAIBE KUKU ILI KUJIKIMU. Mungu ibariki Tanzania tupe nguvu ya kuendelea kupambana bila kuchoka na hawa mafisadi wanaoendelea kutuibia bila huruma !! AMEN
Swali langu kwa Mh. Raisi Kikwete: Je ulipoapa na tena ukashika msahafu na pia Katiba ya nchi, je, uliapa kulinda mali na rasilimali za Tanzania au ni kuziweka chini ya wageni na hasa mafisadi ambao sasa wanaendelea kuitafuna tanzania bila kushibisha matumbo yao ? Naomba utafakari haya na ukiendelea kuiweka Tz chini ya mafisadi, miaka 5 siyo mingi. Watanzania tutakuhukumu siku moja kwenye mahakama zetu au zile za kimataifa !!!!
M. Abdallah Salehe