Tume yataja sababu za watotokukosa elimu

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Elimu duni pamoja na mila potofu zinasababisha watoto wengi walio chini ya umri wa miaka 18 kukosa kupata haki yao ya kielimu.
Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Francis Nzuki, alisema hayo alipozungumza na NIPASHE ofisinikwake, jijini Dar es Salaam jana.
Alisema wazazi au walezi wachache kukosa elimu na kuthamini mila na desturi potofu,kumesababisha kuongezeka kwa watoto wengi wanaokatisha masomo baada ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi.
Huu ni ukatili kwa watoto, kwani kuna baadhi ya mila na desturi ni potofu hapa nchini ni lazima zikemewe, kutokana na baadhi ya wazazi au walezi kudhani kuwa, mara mtoto wakeanapopevuka anapaswa kuoa au kuolewa, hii si sahihi na inasababisha kukatishwa masomo na kuporomoka kwa elimu. Pia inanyima haki mtoto kupata elimu, alisema.
Alisema Tume ilianzisha dawati lawatoto kwa ajili ya kupokea taarifa zinazohusu haki za watoto, ikiwamo elimu, na kisha kuzifanyia kazi taarifa hizo.
Utafiti wa haki za watoto wa mwaka 2006 unaonyesha kuwa watoto wengi wako chini ya miaka 18 wanafanyiwa ukatili, na hivyo Tume iliendesha hoja hadharani ili kupata ufumbuzi watatizo hilo.

CHANZO: NIPASHE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…