Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Kwa kipindi cha hivi karibuni kwenye maeneo mbalimbali nchini hususani ndani ya Jiji la Dar es salaam kumekuwepo na wimbi kubwa la kuenea kwa taka za chupa za plastiki za rangi hasa zinazotokana na vinywaji vya 'Energy drink' hali ambayo inaendelea kushamiri zaidi.
Katika uchunguzi wangu ambao nimeufanya kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, nimebaini kwenye kila hatua tano hadi 10 kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na chupa hizo.
Lakini katika hali ya kushangaza zaidi chupa hizi unazikuta hata kwenye mitaro ya maji hali ambayo inapelekea plastiki hizo kusafirishwa mpaka kwenye vyanzo vya maji na kupelekea kuweka hatarini uhai wa viumbe vinavyoishi kwenye maji pamoja na afya ya binadamu ambao wamekuwa wakitegemea vyanzo hivyo kupata huduma mbalimbali ikiwemo maji na samaki.
Naweza kuwa nipo sahihi kwa asilimia kubwa kusema kwamba, Jiji la Dar es Salaam kwa sasa ni kama limepambwa na chupa za rangi za plastiki, na sababu ni kutokana na chupa hizi kuonekana kila kona kama sio kila upande.
Suala hili limenifanya nirejee kauli ya aliyekuwa Mkurugenzi wa NEMC,Dkt. Samuel Gwamaka Mafwenga ambayo alitoa Mwezi November 2023 akiwataka wazalishaji wa bidhaa zinazotumia chupa za rangi kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kurejeleza chupa hizo ili zisiendelee kuharibu mazingira.
Pia baada kusikiliza kauli hiyo niliamua kupitia miongozo mbalimbali kuona inaelekeza nini kwenye suala kama hili linalogusa ustawi wa mazingira.
Miongozo hiyo kuanzia kwenye Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021, mwongozo wa uthibiti wa taka ngumu kwa kutumia dhana ya punguza, tumia tena na rejeleza wa mwaka 2021 pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 kwa ujumla wake inawataka wazalishaji wa taka hususani wawekezaji kushiriki kulinda mazingira kutokana na bidhaa wanazozalisha kwenda sokoni hasa zile zinazoweza kurejelezwa.
Kimamlaka nchini waliopewa dhamana ya kusimamia utekelezwaji wa Sheria na miongozo hiyo ni Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), lakini jambo la kushangaza zaidi suala la chupa za rangi kuzagaa mtaani limekuwa la kawaida na hatusikii wazi wahusika wakiwajibika licha ya kero hiyo, jambo ambalo linaacha maswali.
Unaweza kujiuliza kwamba hivi wahusika ambao ni wawekezaji wenye viwanda vinavyozalisha chupa za rangi wapo juu ya Sheria au mamlaka zimekosa meno ya kun'gata (kuwawajibisha kuzingatia Sheria na miongozo).
Kinyume na hivyo labda kama kuna jambo nyuma ya pazia, maana hali sio shwari hii ni kero ambayo kama haitapatiwa ufumbuzi wa haraka Dar es Salaam na maeneo mengine hususani ya majiji na miji yatazidi kupambwa na taka hizo ambazo ni hatari kwa ustawi wa mazingira.
Kama NEMC wamekuwa wakitoa matamko lakini hali bado ni changamoto basi mamlaka za juu zaidi kupitia Wizara yenye dhamana haina budi kuchukua hatua ya kufuatilia nini kinakwamisha uwajibikaji stahiki ili kama kuna uzembe kwa wasimamizi wa Sheria na miongozo au wazalishaji wawajibike ili mazingira yetu yaendelee kubakia salama japokuwa tumechelewa.
Ni muhimu viwanda vinavyozalisha chupa za rangi hasa vinywaji vya 'energy drink' kuhakikisha vinakuwa na teknolojia rafiki ya kurejeleza taka zinazotokana na bidhaa baada ya kwenda sokoni, na hili linatakiwa kuwekewa mkazo zaidi na kusimamia kwa ukaribu.
Tamko lililotolewa na NEMC, Novemba 2023
Pia Soma:
~ NEMC imetoa mwezi mmoja kwa viwanda vinavyozalisha Chupa za plastiki zenye rangi kuweka utaratibu wa kukusanya na kuhifadhi chupa hizo
~ Mo Dewji asema wameanzisha Kampeni ya kukusanya chupa za rangi nyeusi, wameshakusanya tani 21
~ NEMC ipige marufuku chupa za plastiki za rangi kuzalisha bidhaa kama energy drink