Tumechoka kubughudhiwa

Tumechoka kubughudhiwa

Joined
Dec 5, 2009
Posts
65
Reaction score
23
Toka mwaka 2006 Tanzania imekuwa nchi ya kusikiliza habari za migongano ya kisiasa baina wabunge na viongozi kadhaa wanaopenda kutangazwa na vyombo vya habari.

Wametokea watu ambao wana kiu sana ya kupigiwa makofi bila kufanya kazi nzito za kujenga siasa na uchumi wa nchi. Hawa ni watu wa hatari sana. Kazi yao ni kuwabomoa wengine tu. Katika siasa hakuna kazi rahisi kama kukosoa. Kila mwenye uwezo mdogo wa kubuni mambo mapya anakuwa busy kuchambua wanayofanya wengine na kuyakosoa tu basi. Yeye hafanya lake bali anasubiri wenye vichwa wabuni mambo halafu wao wayachambue na kuyachallenge.

Kumetokea kundi linalotaka jamii iwaheshimu kwa kupambana na ufisadi. Eti wao wanawashambulia watu wanaoitwa mafisadi. Kwanza fisadi ni nani? Nani anathubutu kumwita mwingine fisadi? Nani anajiona kuwa yuko kwenye siasa na yeye ni msafi kabisa?

CCM ni imara kutokana na mshikamano wake na wafadhili wa chama. Huu ndio msingi wa ushindi wa mara kwa mara wa Chama Cha Mapinduzi. Wanaofikiri kuwa CCM inashinda kirahisi waulize siasa zilivyo. Watu leo wanapiga kelele Fisadi Fisadi Fisadi fisadi. Mbona leo ndo wanaona fisadi. Kwa nini hawakuona fisadi mwaka 2005 wakati wanaomba misaada kwa ajili ya kampeni kwa majimbo yao. Wamesahau tumefuel gari zao zote za kampeni na zaidi ya watu mia moja wako katika bunge kwa ufadhili wa wapenzi wa chama. Wale wanapenda chama toka kwa moyo yao wamekiwezesha kushinda kwa kishindo.

Wanaona fisadi leo, hawakuona mwaka ule wa uchaguzi 2005. Wanatangaza kuwa wafadhili wanaua chama. Chama hakiuawi na wafadhili kinauawa na waroho, wanaotaka umaarufu wa chee!!

Wanaotaka tuondoke katika chama hawajui siri za chama hata kidogo. Wao wataondoka watuachie chama tuendelee kuongoza nchi hadi mwisho tulete maendeleo kwa watu wote wa Tanzania. Sasa watu wanazungumza kuunda chama wakati watataka pesa kuunda chama kifikie nguvu ya kushinda uchaguzi. Si rahisi kushinda maadui wa nje kabla ya kushinda fikra zako inferior. Hawawezi kwenda chama ingine vya siasa maana yote imekwishamalizwa nguvu yake.

Wawache majungu rudini katika moyo ule mmoja wa kupenda chama chetu CCM tukiimarishe tushinde tena uchaguzi huu kwa kishindo.

Those who wish to think positive are always positive movers: even when they face challenges they take them positively.
 
Tutakapoamua kujibu mapigo hapatatosha hapa. Kila mtu ni mfisadi tu humu
 
We!! Weeeeee!!
Ishia hapo hapo. Usivuruge nyongo zetu tuanze kuzitapika hapa
 
Back
Top Bottom