benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amegiza Bodi ya Wakurugenzi ya Bohari ya Dawa (MSD) kufumuliwa na kusukwa upya ndani ya miezi sita hilo likienda sambamba na kuondoa watumishi waliokaa zaidi ya miaka 20.
Waziri Ummy amesema kumekuwapo na tuhuma kubwa za rushwa MSD na licha ya kuondoa wakuu wa idara bado kunahitajika mabadiliko makubwa illi kuiunda upya. Ikumbukwe hii sio mara ya kwanza kwa serikali kutoa maelekezo ya kufumua MSD, mara kwa mara maagizo ya kuifumua MSD yamekuwa yakijirudia.
Mei 9, mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alifanya ziara MSD na kuagiza watuhumiwa wote wa ubadhirifu kama ulivyoainishwa na CAG wachukuliwe hatua, huku akiahidi kuwa TAKUKURU inafanyia kazi hoja zote zilizotolewa kuhusu bohari hiyo.
Aprili 14, mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan, alimteua Ofisa Mwandamizi wa Kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PWC), Slaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, pia alimteua Kiongozi Mkuu wa mradi wa USAID Global Health Supply Chain Technical Assistance, Ali Tukai, kuwa Mtendaji Mkuu wa MSD.
Rais Samia akitaka uwajibikaji kwa MSD ili kuwahudumia wananchi hasa kwa kupata dawa na vifaatiba muhimu kwa kuwa serikali inaelekeza fedha nyingi eneo hilo.
Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia, yalifanyika siku chache baada ya CAG, kubaini bohari hiyo ilishikilia zaidi ya Sh. bilioni 14 za hospitali kwa mwaka mzima bila kupeleka awa na vifaa tiba. Pia alibaini MSD ilifanya ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni tisa bila mkataba halali, pia ilifanya malipo ya Sh. bilioni 3.52 kwa wazabuni sita bila kufuata taratibu na kuitaarifu Bodi ya Zabuni ya MSD.
Aidha, walifanya zabuni 23 zenye thamani ya Sh. bilioni 8.55 nje ya mfumo wa ununuzi wa umma kwa mtandao (TANePS) unaosimamiwa na Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), kinyume na ma- takwa ya sheria.
Walifanya malipo ya awali kiasi cha Sh. bilioni 14.89 kwa wazabuni watano bila mkataba wowote wa makubaliano mengine ambayo yali- bainisha msingi wa malipo ya awali. Aidha, waliendesha mchakato wa ununuzi na kutoa mkataba wa kusambaza Liquid Syrup' wenye thamani ya Sh. milioni 989 bila kush- irikisha Bodi ya Zabuni ya MSD. Pia walitumia Sh. milioni 215 kugharamia posho ya watumishi watatu waliokwenda China kwenye majadiliano ya kuleta mashine za Dialysis kwa siku 61.
Waziri Mkuu, Majaliwa alivyotembelea alisema walibaini kuna udhaifu wa usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi licha ya kwamba wamelipwa. Katika idara ya ununuzi walibaini kuwapo watumishi ambao sio wataalamu na kuagiza wote 16 kuondolewa na kuwekwa watumishi wenye taaluma hiyo. Kwa maelekezo hayo, inadhihirisha kuwa kuna tatizo kubwa ambalo hata serikali inaliona ni wakati wa kufanya uamuzi ambao utakwenda
kuondoa ufisadi unaodaiwa kuwapo.
Tayari CAG amethibitisha kuwapo kwa upigaji mkubwa, lakini hatua ambazo zimeendelea kuchukuliwa ikiwamo kubadilisha uongozi wa juu wa bohari bado hazijasaidia na sasa waziri anaeleza uwapo wa upigaji uliokithiri.
Tunaamini maelekezo ya Waziri Mkuu ni ya juu zaidi kuliko ya Waziri wa sekta husika.
Na pia tunaamini Waziri wa Sekta kuja na maelekezo mengine kabla ya kueleza yale ya awali yaliyotolewa na Waziri Mkuu utekelezaji wake umefikia wapi sio jambo zuri, hivyo ni muhimu serikali ikachukua hatua za utatuzi wa kudumu kuliko kuendelea kuja na maelekezo juu ya maelekezo
Kama tatizo limeonekana basi lishughulikiwe kwa kutumia mihimili muhimu ya serikali ambayo inaona kila mahali ili kuondoa majadiliano ya mara kwa mara kuhusu MSD kukosa vifaa tiba na dawa.huku wananchi wakiumia kwa kukosa vifaa tib ana dawa.
Disclaimer: Sehemu kubwa ya andiko hili imetoka kwenye Gazeti la Nipashe toleo namba 0581019