Tumefanya nini kuzuia Misitu yetu isiangamizwe kwa Mkaa (Mazingira)?

Tumefanya nini kuzuia Misitu yetu isiangamizwe kwa Mkaa (Mazingira)?

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Ningetamani kuwe na mpango mahsusi wa kushusha bei ya Gesi na kuisambaza ifike Vijijini ili tupunguze uharibifu wa misitu.Naamini tunaweza pia kusimamia Shirika letu la umeme liwe na faida na kuweza kusambaza umeme wa bei nafuu.
TANESCO waache kuamini kuwa, watapata faida kwa kuhudumia wateja wachache kwa bei ya juu.

Biashara ya ulimwengu wa sasa ni kuuza kwa watu wengi kwa faida kidogo. Hivi makaa ya Mawe hayawezi kutumia kwenye Taa sisi kubwa kama jeshi, Magereza na mashule kama mbadala wa kuni/mkaa? Binafsi naona bila mbinu mbadala ya kuwapatia watu Energy; mbinu zozote za kuzuia watu wasichome mkaa zinakuwa za kupoteza muda na kutumia gharama bure ambapo matokeo yake hayata onekana.

Naomba mawazo yako
 
Kuhifadhi misitu bila kukata mkaa ilikuwa hoja ya kwanza ya jk alipoingia ikulu,hakufaulu kwa sababu haufikiria mbadala wake ni nini!
 
Ikumbukwe kuwa ajira sikuhizi ni tatizo, kwahiyo misitu inateketezwa kutokana na hitaji la ardhi kwaajili ya kilimo kama mbinu mbadala ya kujikwamua kiuchumi. Katika process ya kusafisha shamba ndipo mkaa unapopatikana.
Mkaa utaendelea kutumika tu hata ikulu wanatumia mkaa ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom