Je tumefika mahali ambapo tulitaka kufika kama Taifa? Je hapa tulipo ndipo wazazi wetu waliposimama kulilia uhuru na kuwa Taifa walitarajia ndipo tungekuwa? Je hapa tulipo ndipo kwa haki yote ndiyo hasa tumepaswa kuwa na siyo zaidi? Je kuna kitu ambacho tungekifanya ambacho kingetufanya tuwe zaidi ya hapa tulipo? Nazungumzia kitaifa katika nyanja zote; elimu, afya, miundo mbinu, huduma za jamii, n.k je tumefikia mahali bora zaidi na tuone fahari au kuna maeneo ambayo hatuna budi kujiuliza kwanini hatujafika mbali?
Ukiangalia changamoto zote tulizo nazo leo hii, bila ya shaka kuna makosa yamefanyika au mapungufu fulani ambayo yawezekana kabisa yametuzuia kufikia pale ambapo tungefikia kama tusingekuwa na makosa au mapungufu hayo. Unafikiri imekuwaje tumefikia hapa tulipo? Na tufanye nini ili tujinasue?
Ni dhahiri ndugu MWKJJ kwamba hali tuliyokuwa nayo, ni hali mbaya na inatisha sana
kwa uchache wa niliyoyagudua hali yetu ni mbaya kwa sbabu zifuatazo.
1:Bado Watanzania hatujazitumia nguvu zetu ipasavyo
Nikiwa nimeishi katika mikoa ya pembezoni mwa ziwa victoria ,nimeshuhudia jinsi mikoa hiyo ilivyokuwa na mvua nyingi na ya kutosha, lakini jiulize ni kwa namna gani tunazitumia mvua hizo?. almost ni mara moja tu kwa mwaka mtu analima kwa nguvu, na siku zilizobaki anakula alivyovitunza kwenye ghala au kuuza ,misimu mingine ya mvua mtu wala halimi .ghafla ikitokea msukosuko akiba haitoshi, laiti tungekuwa tunalima kisawasawa ,tungepata chakula cha kutosha na pia tungeuza vile vya kuuzwa.
2:Kuiga mfumo wa Elimu wa Wazungu
Chukulia pale mlimani Kozi kama ya Computer Engineering, Computer engineer anaweza kudesign na kutengeneza computer/component zake, lazima ziwepo lab za nguvu na vifaa kiujumla, Wazungu wanavimudu vitu hivyo na nchi zao zina makampuni kibao ya wanafunzi wao kufanyia field, sisi kwetu mwanafunzi wa computer engineering anakwenda kufanya Field Celtel/TTCL, jiulize wapi na wapi tutaweza kupata maengineer walioiva kikweli kweli?
3:Mazingira mazima ya Ukuaji wa Mtoto ni Utatanishi
hatuna sera ya kuelezea tufanye nini kwa mtoto wetu kila anapopiga hatua ya ukuaji.
Jukumu la namna gani mtoto alelewe limeachiwa mzazi peke yake, hatuna sera ya kitaifa yenye kutoa muongozo wa kumsaidia mzazi kuonyesha kwamba kila mtoto akifikia hatua fulani basi afundishwe vitu kadhaa, au mtoto katika hatua hiyo ya ukuaji awe anajua vitu kadhaa, mathalani kuna viwango standard kwamba mtoto akiwa na miezi kadhaa lazima awe na uzito fulani.lakini hakuna viwango vilivyowekwa kumsaidia mzazi kumuongoza katika kukuza viwango vya ufahamu vya watoto wao. Yaani imekuwa kila mzazi/mlezi na lwake. sasa mtoto huyu ambaye kutokana na kutokupewa mwongozo imara wa ufahamu bora(ukiondoa elimu ya darasani ambayo ni dhahiri peke yake haitoshi)anakuwa hajaandaliwa kuwa askari mahiri wa kupambana ipasavyo katika challenge nyingi za maisha, maana kuna mambo mengi, kujiajiri, kujilinda na maradhi ya maambukizi, kuepuka uvunjaji wa sheria, ndoa, n.k
4:Uongozi kugeuka kuwa ni biashara
Mtu haiingii katika siasa kutokana na uchungu wa Wananchi, mtu anaingia katika siasa kwa utashi kwamba akipata uongozi aitumie nafasi yake kujinufaisha, kwa kujipa tenda, kuvizia posho na luxury nyingine, kuingia mikataba mibovu ili mradi awe amekula, n.k
hayo ni baadhi tu