Tumehamasishwa sana kuwa na bima za afya na kuielewa serikali; mbona dawa mhimu kwa jamii zimeondolewa kwenye bima ya afya hi?

Tumehamasishwa sana kuwa na bima za afya na kuielewa serikali; mbona dawa mhimu kwa jamii zimeondolewa kwenye bima ya afya hi?

Asante sana mleta mada kwa kuleta taarifa hii. Siyo hii tu hadi steipes za sukari wamezitoa yaani bima vile haina msada tena kwa wateja. Item zilizotolewa ni 180 na sio 18.
 
Asante sana mleta mada kwa kuleta taarifa hii. Siyo hii tu hadi steipes za sukari wamezitoa yaani bima vile haina msada tena kwa wateja. Item zilizotolewa ni 180 na sio 18.
Kwa maana nyingine watu wenye mahitaji ya hizo dawa na wanalipia Bima za afya kama hawana pesa ndio umauti unawajongelea!
Kwa hivi sasa vyombo vya kutetea wateja naona kama taasisi zinazohusika na kudhibiti uendeshaji wa mashirika vimepatwa na paralysis. Hivi taasisi inaachwa ili imalize watu bila ya chombo kinachodhititi uendeshaji wa Bima kufata mchakato wa malalamiko? Hivi wawakilishi wetu Bungeni wanaliona hilo? Au mpaka mheshimiwa Rais aingilie kati kama alivyofanya kwenye kikokotoo?
 
Furosemide ndio hiyo hiyo Lasix. Sasa mara unasema imetolewa na hapo hapo unasema inabaki
 
NHIF ni jipu kubwa sana, Mh. Rais wangu naomba uende pale Kurasini NHIF HQ plz, madudu yao ni mengi sana
 
Relax ndugu. Hayo marekebisho sio rasmi. Utekelezaji wake bado. Na msingi wa wao kuleta mapendekezo hayo sio wao kama wao NHIF, ni hao hao politicians.
 
Kuna mtegemezi wangu alinyimwa dawa alizokuwa akitumia na kuambiwa Sasa dawa haiko kwa Bima!
 
Bima ya Afya ni mfumo wa kumwahidi kumrejeshea mwanachama hali ya Afya bira malipo pindi anapopata shida ya kiafya kwa kuuugua au kulazwa hospitalini hasa pale tu anapokuwa amelipia michango ya marejesho (premiums) kila mwezi au kwa mwaka.

Huko nyuma hasa miaka ya kuanzia 2010 kurudi nyuma; watu wengi walikuwa hawana elimu ya umuhimu wa Bima ya Afya. Hospitali nyingi zilikuwa hazipokei Bima ya Afya isipokuwa za Serikali na baadhi za watu binafsi. Pia mgonjwa mwenye Bima ya Afya alikuwa hapati huduma ya kurudhisha na ilikuwa si ya haraka kwani inasemekana alikuwa akithaminiwa mgonjwa mwenye Cash! Pia dawa nyingi zilikuwa hazijawekwa Kwenye Bima.

Hali hii iliwafanya watanzania kuidharau Bima na kutoona umuhimu wa kuwa nayo au kuwakatia wategemezi.

Kwa kipindi kirefu sasa toka miaka hiyo; Bima ya Afya ilikuwa imejizolea umaarufu sana na kupendwa na we ananchi kwani mgonjwa mwenye Bima ya Afya alikuwa akijisikia Fahari kuwa na Bima kwani hudumu zilikuwa Bomba. Dawa Kama zote zilikuwa zimewekwa Kwenye Bima. Pia kupitia tangazo la Serikali na mkazo wa Dada yetu Ummy Mwalimu la kuhamasisha watu kuwa na Bima za Afya; wananchi wengi waliona umuhimu wa kumiwa nayo.

Bima za Afya Kama NHIF; STRATEGIS, AAR, NSSF na ICF zimekuwa kimbilio kwa wananchi na kuwa mkombozi wao kwa huduma za matibabu. Hudumu ni nzuri tena ya kwaminika. Baadhi ya hospitali za Serikali na binafsi wamefanikiwa kutenganisha kabisa Vitengo vya matibabu; yaani kitengo cha wagonjwa wenye Bima za Afya na Kitengo cha wagonjwa wenye Cash. Na hii imekuwa msaada sana kwa matibabu. Hongera sana!

Kipindi hiki; wewe ni mtanzania gani ambae huna Bima ya Afya? Kila mtu atakushangaa na kukuonea huruma endapo umepatwa na tatizo la Afya au mtoto waki ama ndugu yako ameugua na huku ukiwa huna Bima ya Afya huku mfukoni huna hata Mia! Happy ndo utauona rangi zote!

Baada ya utangulizi huo,sasa niende Kwenye maada husika isemayo: " Tumehamasishwa sana kuwa na Bima za Afya na kuielewa Serikali; Mbona Dawa Mhimu kwa Jamii Zimeondolewa Kwenye Bima ya Afya!"
Ni kweli kuanzia mwezi ulopia Kama si mwezi wa nane, orodha ya dawa Kama 18 za magonjwa ya Pressure na Kisukari yameondolewa kwenye Bima.

Dawa hizo ni zile nzuri kweli kwa watumiaji kwani ndo zinazoonekana kuleta nafuu na kunesha kwa baadhi ya wagonjwa. Yaani hushusha au kupandisha fasta Presha na sukari. Hureta good regulation ya magonjwa hayo.
Wahenga walisema kizuri kina gharama; ni kweli dawa hizo ni za bei sana kwani huuzwa kwa Bei ya juu. Za Presha huuzwa hata tsh 36000 na zaidi kwa vidonge 30!

Kama wewe una Presha au Kisukari ama una ndugu; jirani au jamaa ana magonjwa hayo na ulikuwa unatimia kati ya Hizi dawa Sasa hutozipata yen bure kwa Bima Sasa utakuea unalipa Cash.
Dawa zenyewe ni Hizi Happ.

A. Dawa za Presha.
Dawa za Presha zilizoondolewa Kwenye Bima ni:

1. Bisoprolol Fumarate 5mg
2. Bisoprolol Fumarate 10mg
3. Termisatan 40 mg
4. Termisatan 80 mg
5. Termisatan 120 mg
6. Concor 5 mg
7. Concor 10 mg
8. Benicar 5mg, 10mg
9. Hydrochlorothiazide
10. Benicar
11. Lopressor
18. Furosemide
.....

Nb: Dawa zilizobaki Kwenye Bima ni Kama
- Lasix
- Losatan
- Amlodipine
- Alsatan
.......

B. Dawa za Sukali

Dawa za Presha zilizoondolewa Kwenye Bima ni:
1. Dipeptidyl peptidase
2. Amylinomimetic
3. Dopamine
...
Mleta mada napenda kukusahihisha.
1. Furosemide ndio lasix. Kama ilivyo kwa methyldopa=aldomet, spironoloctone=aldactone etc. Hii ni kwa sababu dawa huwa ziko na generic name pamoja na commercial name.
2. Blood pressure is one of the vital signs and not a disease. When blood pressure deviates from normal and become high above the normal range a person becomes Hypertensive kwa hiyo pressure ni kitu kingine na hypertension ni kitu kingine
 
Mleta mada napenda kukusahihisha.
1. Furosemide ndio lasix. Kama ilivyo kwa methyldopa=aldomet, spironoloctone=aldactone etc. Hii ni kwa sababu dawa huwa ziko na generic name pamoja na commercial name.
2. Blood pressure is one of the vital signs and not a disease. When blood pressure deviates from normal and become high above the normal range a person becomes Hypertensive kwa hiyo pressure ni kitu kingine na hypertension ni kitu kingine
Lakini Maada kuu iko sahihi? Je hakuna dawa zilizoondolewa kwenye Bima? This is the matter plz!
 
Mleta mada napenda kukusahihisha.
1. Furosemide ndio lasix. Kama ilivyo kwa methyldopa=aldomet, spironoloctone=aldactone etc. Hii ni kwa sababu dawa huwa ziko na generic name pamoja na commercial name.
2. Blood pressure is one of the vital signs and not a disease. When blood pressure deviates from normal and become high above the normal range a person becomes Hypertensive kwa hiyo pressure ni kitu kingine na hypertension ni kitu kingine

Vitu vingine unavipotezea tu mkuu hatakama ni unajua sana cha msingi tu angalia ujumbe zaidi hizo mbwembwe nyingine sijui normaltensive , hypertension , blood pressure , tuachie sisi
 
Bima zote za afya zinabagua kutoa dawa nzuri hata za ngozi.

Ifike wakati Sasa Waziri wa afya aingilie na kusimamia kidete dawa zikubaliwe na bima.mwisho wa siku haitakuwa na maana Kama Nina inatoa Panadol tuu
Huu no utapeli na wizi kwa wananchi na wateja wao.
 
Kikubwa cha kujua taasisi zote hasa za gvt haziko kwa ajili ya kumkomboa mnyonge bali kumnyonya huku wakija na mwamvuli wa kusaidia.angalisia nssf,nhif,nic,tucta yaani ni unyonyaji na mateso.
Usije ukajichanganya kufanya kazi na serikali with ur money.Poleni wana bima.
 
Relax ndugu. Hayo marekebisho sio rasmi. Utekelezaji wake bado. Na msingi wa wao kuleta mapendekezo hayo sio wao kama wao NHIF, ni hao hao politicians.

Sasa atulie wakati hao NHIF ndo watekelezaji, tunapaswa kupiga kelele zote na vyombo vyote vya habari viandike habari hizi
 
Asante Sana kwa Maelezo mazuri sana. Ni kweli kabisa kuwa NHIF wamepunguza baadhi ya huduma walizokuwa wakitoa hapo mwanzo.
NHIF wanawataka Madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya kutoa huduma zilizo ndani ya mwongozo wa taifa wa matibabu (standard treatment guideline), kwa maana nyingine ni kwamba ukiandika dawa isiyokuwepo kwenye huo mwongozo Nhif hawatakulipa wewe mtoa huduma.

Kwa Mana hiyo ndio maana watoa huduma wanakataa kutoa huduma hizo ambazo hawataweza kulipwa na Nhif japokuwa zinasaidia wagonjwa na hata kama Wagonjwa hao walizitumia awali. Watoa huduma wamelalamika sana kwa Nhif lakini nao Nhif wanawarushia mpira wizara ya afya ambao ndio hutengeneza huo mwongozo wa matibabu kupitia kwa wataalamu mbalimbali kutoka hospitali zetu kubwa km muhimbili.

Sintofahamu ipo hapa: pamoja na kuwa nhif hawalipi huduma ambazo ziko nje ya huo mwongozo lakini kwa hospitali kubwa Kama muhimbili, Bugando na kcmc wanalipwa hata kama wakitoa huduma kwa Wagonjwa zilizo nje ya mwongozo huo pia Nhif imeweka tabaka la maafisa ambao wao watatakiwa kupewa huduma yoyote bila kujari ipo kwenye mwongozo wa matibabu, mfano Wafanyakazi wa nmb, bot, wabunge, mawaziri and the like.
So hiyo issue ipo hivyo ndg zangu.
 
Hii NHIF wanafanya biashara na wao wanatarajia kutoa gawio kwa serikali kama mashirika mengine kwa hiyo ni lazima wabane dawa za wagonjwa. Kaazi kwelikweli.
 
Kwa kusema haya sitaki kuonekana natetea NHIF. Mimi nitaongelea uelewa wangu juu ya "Insurance Industry" NHIF ni shirika la umma ambalo inafanya biashara ya bima ya afya. Biashara ya bima inafanyikaje? Biashara ya bima ni ya kucheza na probability. Kiasi unachotumia pale unapoumwa kinaweza kikawa zaidi ya kiasi utachochangia. Bima wanakusanya hela kwa kutegemea kwamba only small population ya wachangiaji wataumwa. Ukienda nchi za wenzetu kwanza ile premium inategemea na umri. Ukiwa kijana utalipa hela kidogo sababu probability ya kuumwa ni ndogo. Ukiwa mtu mzima premium inaweza ikawa kubwa sababu probability ya kuumwa inakuwa kubwa. Na jambo lingine wana uwezo wa kukufanyia assesment kabisa kabla hawajakubali kujua risk factors zako.

Sasa hapa kwetu kuna kamchezo kamezuka, unakuta mtu anaenda kukata bima wakati tayari anajijua ana chronic condition, kama kisukari au presha. Kwa wenzetu wakikupima wakakuta tayari una tatizo la presha, basi na premium inaweza ikawa kubwa. Sasa magonjwa haya yanaonekana kuwapata sana watu wazima, lakini huku kwetu hata vijana wa miaka chini ya 40 kwa sababu ya lifestyle. Kampuni ya Insurance ikishakuwa na wagonjwa wengi wa aina hii inakuwa katika risks zaidi ya kupata hasara, yaani asilimia kubwa ya wateja wao wanaumwa mara kwa mara, na magonjwa wanayoumwa yana gharama sana kwenye upande wa dawa. Hapa sasa ndo wanaanza kutengeneza hizo exclusion criteria kuondoa dawa za magonjwa ambayo ni chronic hasa pale idadi ya wagonjwa inapokuwa kubwa sana.

Pia jambo lingine wanachofanya kwenye insurance industry ni kuweka ceiling ya kiasi ambacho wapo tayari kulipa kwenye bili. Na hii ni kwa kampuni nyingi za bima duniani. Hivyo ndiyo strategy ya industry ya bima ilivyo. Ukitaka kujua kwamba bima wanaoperate kwa kuassess risk, we angalia kwanini kwenye "primary agriculture" bima zinakuwa hamna au kama zipo premium ni kubwa sana. Sababu kuu, ni kwamba kilimo kina risk kubwa ya majanga. Mfano mazao yanaweza kuharibika wakati wa kutafuta soko au yakaharibia shambani kutokana na mvua iliyopitiliza au mvua kuwa chini ya wastani. Hivyo ndivyo bima ilivyo. Kwa watu walisomea haya mambo wanaweza kufafanua zaidi.
 
Back
Top Bottom