Tumehifadhi namba za simu za watu waliofanikiwa tukidhani ni msaada kwetu

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
MHADHARA (100)✍️
Sisi masikini tunahifadhi namba za simu za watu ambao wamefanikiwa kimaisha na wengine wameinuliwa kwenye nyadhifa mbalimbali za uongozi. Tunafanya hivyo tukidhani kwamba siku tukipatwa na shida yoyote watatusaidia.

Wakati mwingine tunawapost mara kwa mara kwenye akaunti zetu (status) za mitandao ya kijamii ili kujionyesha kuwa tunajuana nao, au kuwapa sifa ili kama kuna uwezekano wowote watukumbuke kwenye mavuno yao.

Hata hivyo ukipatwa na shida yoyote unagundua kwamba watu wanaokusaidia kwa haraka ni wale unaofanana nao hali ya maisha. Ishi vizuri na watu ambao unafanana nao hali ya maisha.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
 
Kila mtu ana umuhimu wake katika Maisha unafikiri mgekuwa masikini tu ingekuaje?
 
Bora wewe namba za simu. Sisi tuna magroup ya kila harusi tukizani watakuja kutusaidia
 
Marafiki na ndugu huja penye Neema,Na mwenye Neema awe mtoaji, wengine ni majanga hata salamu tuu hapokei!
 
Upo sahihi sana, Hatua ya kwanza ondoa mentality ya kutaka kusaidiwa, ikitokea umesaidiwa iwe ziada tu. Kuwa tayari hata kufa if that is the only option.
Huyo aliyefanikiwa unafikiri ni wangapi wanamuangalia kama msaada? chances za kukusaidia wewe katika wengi ni ngapi?

The only option to avoid disappointments is avoiding expectations.
 
Hizi mentality za kutaka kusaidiwa zipo kwa waafrika tu.

Ukija kwa wazungu, kila mtu anakufa na tai yake shingoni.

Kusaidiana kuna lemaza na ku feel kwamba una haki ya kusaidiwa.

Huu ujinga haupo kwa nchi zilizoendelea.

In the jungle of life salvation is largely on your hands.
 
Naona watu wengi nyuma ya keyboard ni mabepari. Hawajui kwa nn misaada inazolewa, umaskini haujatokea tu from nowhere, kuna sehem umezaliwa. Na walioko juu wanalazimika kubust hawa wa chini sabab umaskini na utajiri ni pande mbili za sarafu moja. Ukichunguza vizuri kuna binary opposition yani kuna sabab zinazopelekea umaskini na hizohizo ndizo zinazozaa matajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…