A
Anonymous
Guest
Mimi ni Mwanafunzi nimehitimu katika Chuo cha Mipango Dodoma Mwaka 2024, changamoto tuliyoipata ni kwamba baada ya Serikali kutuongezea hela ya ada Wanafunzi tuliyokuwa tumeshalipa hatujarudishiwa fedha ambazo tulitakiwa kupewa as ‘refund’.
Tulitakiwa kulipwa tangu Julai au Agosti 2024 lakini mpaka leo hakuna kitu licha ya kufuata utaratibu wote uliotakiwa ikiwemo kujaza karatasi za malipo.
Wakati wa graduation walituambia tujaze karatasi fulani kisha wakasema tutaanza kulipwa ndani ya siku tatu, hiyo ilikuwa tarehe 20 au 21 Novemba 2024.
Hatujui nini kinachokwamisha wao kutulipa licha ya kuwa kila kitu kimeshakaa sawa na sisi tumeondoka chuo, inavyoonekana tukikaa kimya hiyo itakuwa imetoka na hatutaweza kupata tena.
Natoa wito kwa Uongozi wa Chuo cha Mipango Dodoma kufanyia kazi suala hili kwani limekuwa kero.