Tumeielewaje katiba?

Tumeielewaje katiba?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Nimekaa kisha nikaona.mwisho wa siku hii katiba itawachanganya wengi. Awali tulikuwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo ilikiwa ni ya serikali mbili; Tanzania bara na Zanzibar. Katiba iloyotimika ilikiwa inajieleza kuwa iliongelea Muungano bila kugusa Tanganyika wala Zanzibar. Leo tayari wazanzibar wana katiba yao. Kwa mujibu wa rasimu ya sasa ni kwamb Tanganyika nayo inatakiwa kuwa na katiba yake. Rasimu ya sasa inasema kuwa kutakiwa na mambo saba yatakayoshughulikiwa na Muungano. Mengine yatashughulikiwa na washirika wa Muungano ambao ni Tanganyika na Zanzibar. Sasa napenda kujua, na wengine pia wangependa kujua kwamba hizi ibara kwenye rasimu zinamuhusu nani? Je zinahusu tu yale mambo saba ya Muungano au yataingilia na utendaji wa majukumu ya washirika wa Muungano?
Mathalan tunambiwa kuwa kutakuwa na wizara 15, wabunge 75, n.k. Hapo si bado wabunge na wizara za washirika wa Muungano? Wajibu wa rais unaozungumziwa humu si wajibu wa rais wa Muungano? Rais asiye na
rasilimali ambaye katiba imemzungumzia kwa mapana.
Kama pakiwa na wizara 15 za Muungano, Tanganyika kutakuwa na wizara ngapi? Haya ni baadbi tu ya maswali ambayo mtu angependa kujiuliza. Kama mawazo yangu ni sahihi, basi naungana na wanaopinga muundo wa serikali tatu maana ni mzigo kuliko maelezo. Na hiyo tume ya katiba kweli imekaa na kupitisha haya?
Jana nizmemsikiliza Prof Kabudi mjumbe wa Tume ya katiba katika kipindi cha Kipima joto itv. Pamoja na mambo mengine alisema kuwa katiba za Ghana na Kenya zilitungwa na jopo la watu tisa tu! Ikaletwa kwa umma kutazamwa na kutolewa maoni kisha kjpitishwa kuwa katiba rasmi katika nchi husika. Kabudi anausifia utaratibu uliotumika nchini kwamba mchakato ulihusisha wananchi wenyewe. Alikuwa akisema kuwa yaliyoko kwenye rasimu ni mawazo na mapendekezo ya wananchi wenyewe. Nikimsikia mara kwa mara Jaji warioba akisema wakati akiwasilisha rasimu ya katiba pale karimjee kuwa 'tume imependekeza'. Alikuwa na maana gani? Kabudi anasema rasimu ni zao la.wananchi kwa asilimia zote. Kulikuwa na haja gani ya kuunda tume ya katiba ambayo mwisho wa siku tume iliamua kupendekeza? Kama ni maoni ya wananchi iweje sasa maoni hayo yaanze kupingwa tena na umma? Ingekuwa heri kama ile tume ya warioba ingejifungia sirini ikaja na rasimu ambayo tungwegawiwa kwa ajili ya kuipitia na kutoa mapendekezo. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom