SoC04 Tumeipokea Polisi Jamii na sasa tunahitaji muendelezo!
Tanzania Tuitakayo competition threads

PamojaNasi

New Member
Joined
May 2, 2024
Posts
3
Reaction score
4
Wasalaam mabibi na mabwana, kaka na dada zangu, awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa uzima na afya, pia nawashukuru sana waandaji wa hili jukwaa la Jamii Forum Story of Change. Kabla ya yote nilipongeze Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo wanajitahidi kuifikia TANZANIA TUITAKAYO!

CHUMBA CHA MASHTAKA.
Naam.. Kabla sijajikita moja kwa moja kwenye mada husika basi naomba nitoe maoni hasa kuhusu chumba cha mashtaka (Charge Room Office) au kwa lugha zoelefu hupaita counter! Nimetembelea vituo vingi vya Polisi, muundo wake pale mapokezi huwa unanipa ukakasi na jaka la moyo.

Vuta picha umeshambuliwa, umetukanwa, umevunjiwa nyumba, umeibiwa nakadhalika nakadhalika lakini unapofika kituoni kutoa malalamiko unahojiwa ukiwa umesimama, hakuna mahali pa kukaa, hakuna privacy kwa issue zenye kuhitaji usiri, hakuna comfortability wakati wa kutoa maelezo, Askari anakuwa amekaa lakini muhanga anakuwa amesimama! Naliomba Jeshi la Polisi kupitia jukwaa hili la Story of Change nalo likabadilishe muundo pale mapokezi na kuwepo na chumba cha ziada kwaajili ya kutoa na kuchukua maelezo chenye viti, meza na mazingira ambayo yatamponya moyo huyu muhanga hata Kabla kesi kufunguliwa! Sambamba na hili matumizi ya lugha nzuri na ukarimu basi Jeshi la Polisi litafika katika Tanzania Tuitakayo!
Picha chini chanzo Pinterest.com

Upland_Room1_Final-1024x768.jpg
Interior Design Kitchen.jpeg


Terejee katika mada yetu, Polisi Jamii na Maendeleo.

Miaka ya hivi Karibuni tumeshuhudia Jeshi la Polisi kupitia mpango wake wa Polisi Kata au Polisi Jamii likifanya vizuri maeneo mbalimbali ya nchi, dhima kubwa ikiwa ni Polisi na Jamii kushirikiana pamoja katika kutokomeza uhalifu. Kwa kiasi kikubwa dhana hii imeleta matokeo chanya ikiwepo upatikanaji wa taarifa za uhalifu na matukio mbalimbali ambayo Polisi inakuwa ikiyashughulikia moja kwa moja. Nimeshuhudia watu wakitoa taarifa Polisi pasipo kuwa na uwoga kama miaka ya huko nyuma. Lakini pia nimeshuhudia ufatiliaji wa Jeshi la Polisi kutokana na taarifa wanazozipokea kutoka kwa watu mbalimbali. Ni kweli sasa dhana ya Polisi Jamii inafanya kazi.

TUSIISHIE HAPO!! TUNATAKA MUENDELEZO
Katika mazungumzo yangu na Polisi Kata ambao nimebahatika kukutana nao katika maeneo yao ya kazi nimepata kujua hivi sasa Jeshi la Polisi limeajiri wasomi, wabobezi na wataalam katika nyanja mbalimbali kama ujenzi, kilimo, afya, ufugaji, usimamizi wa fedha, uchumi, elimu, biashara, Sheria, Usafirishaji, uhandisi, wasanifu majengo nk. Lakini wataalam hawa hawafanyi kazi katika field walizosomea (Misuse of Power)

Ndipo nikapata wazo la POLISI JAMII NA MAENDELEO, Polisi ukiachana na jukumu lao la msingi la Kuzuia, Kulinda na Kupambana na Uhalifu wanaweza kutumika katika kuleta Maendeleo ya Tanzania Tuitakayo kupitia dhana ile ile ya Polisi Jamii. Mfano huyu Polisi Kata ni mtaalam wa kilimo Cha Umwagiliaji, na katika Kata yake vijana wengi wanaoongoza kwa vitendo vya uhalifu chanzo ni ukosefu wa ajira! Sasa ni wakati wa huyu Polisi Kata kutoa elimu kuhusu madhara ya kuwa muhalifu lakini pia kutumia ujuzi wake wa Kilimo Cha Umwagiliaji kuwafundisha hawa vijana ambao wamekubali kuacha uhalifu na kuwa raia wema kujifunza kilimo na Kisha kujiajiri. Then serikali ya Kijiji ikatoa eneo ambalo vijana hawa wataenda kujifunza kwa vitendo kuanzia hatua ya kwanza mpaka mwisho kwenye mavuno. Naamini Jeshi la Polisi kupitia wataalam lililonao linaweza kushirikiana na asasi za kiraia, wizara na serikali kwa ujumla Ili kufikia lengo.

MY TAKE ni kwamba tusiishie tu katika kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi bali ni muda sasa wa kuunda vikundi vya maendeleo ambavyo vitakuwa vinatambulika na kupewa muongozo kutoka kwa wataalamu kutoka Jeshi la Polisi wakishirikiana na wizara husika, mfano kwenye kilimo basi wizara ya kilimo nayo inatia mkono kwa kuwawezesha vijana hawa kufikia lengo. Kuliko siku nzima unahubiri vijana kuacha uhalifu na ingali tunajua vijana hawa hawana ajira.. basi sasa katika mafunzo hayo kuwe na namna sasa Polisi Kata, Watendaji wa vijiji kuja na wazo la ubunifu Ili kutatua changamoto hizo.Tunawaambia vijana waache kutumia madawa ya kulevya lakini kutokana na stress za kukosa kipato kijana huyu atakusikiliza tu na akitoka hapo ataendelea na madawa yake!

Ni muda sasa wa Jeshi la Polisi kutumia Askari wake wasomi katika field walizosomea Ili kuleta Maendeleo ya Taifa hili. Na hapa tujikumbushe kwamba kazi zote zinafundishika! Vuta Picha Askari ni fundi ujenzi! Maana yake uaskari ni kazi na ufundi ujenzi ni kazi pia! Kama ambavyo anaweza kushika tofali akajenga na huku akashika bunduki kulinda raia na mali zao basi Askari huyu anaweza pia kuwa Askari Kata na bado akawafundisha mbinu vijana ambao ndio kundi kubwa kwasasa kwenye Taifa hili kuondokana na umaskini kwa kujifunza kazi mbalimbali.

Na sio kujifunza tu bali sasa kupitia hawa askari ambao wanaaminika katika kila idara kuwa kama daraja la hawa vijana kujipatia nafasi mbalimbali za kazi mfano, mashambani, miradi ya ujenzi wa majengo ya serikali nk. Lakini pia tumeona Jeshi lenyewe likiwa na uhaba wa majengo na makazi, Wataalam hawa wakitumika vizuri Jeshi la Polisi litaenda kuondokana na hii changamoto.

FAIDA ZA POLISI JAMII KUSHIRIKI KATIKA MAENDELEO.
1. Kiwango Cha Uhalifu kitazidi kupungua. Kutokana na vijana wengi kuwa washirika kamili wa Jeshi la Polisi kupitia miradi mbalimbali ya Maendeleo wanayoshirikiana.

2. Kuimarika kwa hali ya usalama wa ndani kutokana na urahisi wa upatikanaji wa taarifa za uhalifu kutoka kwa Jamii.

3. Kuchangia Maendeleo katika Jamii husika. Kama ambavyo tunasema kazi na dawa, basi itasaidia kazi za Polisi kufanyika lakini pia Maendeleo kupatikana kwa mtu mmoja mmoja au kikundi na Taifa kwa ujumla kupitia vijana ambao wamekubali kuacha uhalifu then kujifunza kazi Kisha kujiajiri.

4. Kuongeza ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na kada nyingine, asasi binafsi na mashirika mbalimbali ambayo yanaweza kuwa yanaunga mkono jitahada.

NB: Kuelekea Tanzania Tuitakayo ni muhimu sana kwa Jeshi la Polisi kushirikiana na Jamii sio tu katika kutoa elimu na kupata taarifa za kihalifu na kuzifanyia kazi bali kushiriki na kuanzisha miradi ambayo itawasaidia hawa vijana ambao ndio kundi kubwa zaidi kwenye uhalifu kuachana na Uhalifu na kuanza kufikiria plan B.
 
Upvote 3
Naliomba Jeshi la Polisi kupitia jukwaa hili la Story of Change nalo likabadilishe muundo pale mapokezi na kuwepo na chumba cha ziada kwaajili ya kutoa na kuchukua maelezo chenye viti, meza na mazingira ambayo yatamponya moyo huyu muhanga hata Kabla kesi kufunguliwa! Sambamba na hili matumizi ya lugha nzuri na ukarimu basi Jeshi la Polisi litafika katika Tanzania Tuitakayo!
Privacy, asee picha uliyoielezea na ulizoambatisha zinafaa sana. Tena sio ya kuishia polisi tu. Taasisi zote zenye sera ya usiri na ziige muundo huu.

Hospitali na zahanati zimeweza. Bado maduka ya madawa (hata kama ni binafsi, imekaa poa aseee) cheki hiii mfano pale OTC. Imekaa poa.


Tukirudi kwenye mada, wazo la kuyatumia majeshi yetu kwa maendeleo ni wazo murua sana.
Maana hatuhitaji kusubiri kupigana vita na wahalifu au wageni. Tunaweza kuishiriki vita iliyopo na inayoendelea na isiyo na uadui wala. Vita ya kiuchumi. Majeshi yetu yoooote yashike nafasi zake katika kutuonesha kwamba katika uchumi wa nchi jeshi lipo njema na linafanya kazi nzuri kujenga uchumi wa nchi.

Mfano mzuri, kilimo -magereza na SUMA JKT, Wapo njema
 
Ahsante kwa mchango wako, Ahsante kwa kuongezea nyama nyama, imekaa poa sana 🙏
 
Back
Top Bottom