Tajiri Kichwa
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 9,021
- 22,016
Kila mmoja anafahamu kuwa tarehe 23 mwezi agosti 2022 kutakua na sensa ya watu na makazi katika nchi yetu. Ni jambo jema maana kwa mujibu wa serikali yetu wanasema inawasaidia wao kutambua wingi Wa watu kwa usawa au mgawanyo wa maendeleo.
Kuna maswali baadhi ya kujiuliza je iyo sensa inatupa taarifa stahiki. Tutazame swala la idadi ya watu. Mujibu tunayosikia idadi ya watu itahesabiwa kupitia maeneo walipolala usiku wa kuamkia tarehe 23 agosti.
Kuna maswali ya kuuliza au kujiuliza vipi wale wanatarajia kusafiri kwenda nje ya nchi hivi karibuni, siku ya sensa itawakuta hawako nchini? Vipi wale walio masomoni karibu mwaka au miaka tunapataje idadi yao.? Je vipi wale wasio na makazi wanaolala barabarani na mitaani? Je, vipi wale madereva ambao hufanya safari zao usiku mfano gari binafsi na gari za mizigo?. Naona kuna kundi kubwa linaenda kukosa haki ya kuhesabiwa.
Je, tumejianda kukusanya idadi tuu au na taarifa muhimu zinginezo, Mfano kufahamu idadi ipi ya watu haijaweza kufikiwa na huduma ya bima.? Je ni watanzania wangapi wametengwa na huduma za kibenki au kifedha? Je ni idadi ipi ya watu waliowekwa nje ya mnyororo wa ajira?
Kwangu sensa naona tunafanya kama ilivyo desturi ya mtu kufanya shughuli ya kumbukumbu kila tarehe fulani inapofika.
Karibu kwa mtazamo au maoni kuhusu sensa. Mfano wewe kwenye dodoso ungependa wakusanye taarifa zipi zaidi.