SoC03 Tumekubali kutawaliwa

SoC03 Tumekubali kutawaliwa

Stories of Change - 2023 Competition

Nsutusu

New Member
Joined
Jun 18, 2023
Posts
4
Reaction score
2
Njia rahisi ya kufanikiwa kwa watu wasio na uwezo wa kujiongoza wenyewe ni kuongozwa mfanowake naufananisha na Mbuzi au ng'ombe ukimpa uhuru atakula majani hata yale ya akiba ya chakula cha kesho, hvyo anahtaji kuongozwa. Hii ni sawa kabisa ukifananisha na afrika, "Kipofu hawezi kuongoza kipofu mwenzie", "usikubali ushauri wa mtu alieshindwa kwasababu atakupoteza", Hii ni baadhi tu ya misemo inayofanana na uhalisia wa mwafrika.

Waafrika hatuna namna tunaweza kujinasua kutawaliwa ni lazima tukubali au tukatae lazima tutawaliwe ndo mambo yaende. Mengi sana tumejidai tunaweza lakini kiko wapi?? yametushinda kila kitu afrika ni wa mwisho usijidanganye wala tusijipe moyo sisi ni wa mwisho.

Kaa chini tafakari hayo mambo. Unayosema Afrika sio ya mwisho tathmini kwa kina uone kama yana umuhimu wowote utakuta hayana mantiki kubwa kiivo.

Tulisema tunaweza kujiongoza saiv afrika ndo mahali pa vita kila leo viongozi wanapinduliwa na hii ni kutokana na uongozi mbovu.

Afrika rushwa imetwala viongozi na sisi wachini tunakubali kutoa na kupokea rushwa tunaona ni kosa dogo.
Tulisema tunaweza kuwekeza tulivyopata tu uhuru viwanda vingi vilianzishwa, leo hii hamna hata kimoja. Tutawaliwe tuteseke kama enzi za utumwa sisi tuwe vibarua kwenye nchi zetu.

Waongeze ugandamizaji haswa kwenye pesa yetu ishuke thamani tuzidi kuwa masikini tukope madeni yasiyolipika.
Kadri tutakavyokua masikini ndivyo tutazidi kutawaliwa kirahisi
Tuna pesa yetu, kila mtu anafuja anavojua mwenyewe, miaka inavyoenda nayo inazidi kupotea tatizo tunakuwa wabishi wa mdomoni lakini vitendo hakuna
Mwanzo tulikuaga na cent 1 cent 2 nk badae zikafutwa zikaja shi 1 sh 2 zikafutwa huu ni ushukaji wa thamani ya fedha mm niliikuta sh 5 na 10 na kuendeleaa zikafutwa saivi inayofata ni sh 50 nayo itafutwa tu maana hakuna kitu utaenda dukani kununua cha maana kwa sh 50.
Afrika ndo sehemu pekee mtu ananunua gari ina km 500,000 laki tano anatangaza amenunua gari jipya.
Sasa afrika ndo soko kuu la malapu lapu yaliyotumika manguo, viatu, simu tumeshindwa kubuni au hata kutengeneza mavazi yetu na kuyaheshimisha.

Afrika ushoga sio utamaduni wetu, saivi nchi za afrika nyingi tu zameukubali ushoga, wengine wanashindwa kuongea kama wanaukubali ama hawautaki. Huu ushoga utakuwa ni pigo moja kubwa sana katika kutawaliwa maana wanaume mtakuwa walaini laini. Kama mimi nawewe tumeshindwa kuukataa ukoloni unadhani kizazi kijacho cha mashoga ndo kitafanya mapinduzi?.

Mala nyingi tunadai kuongezewa mishahara, hatujui kuwa tunaliumiza taifa, kama nguvu ya kudai ongezeko la mishahara ingetumia kudai kuimarishwa kwa uchumi pesa ingekua na thamani hakungekua na haja ya kuongea mshahara. Tutawaliwe waje watuimarishie uchumi wetu.

Afrika kuna nchi ina watu milioni 60 haijawahi kufuzu kombe la dunia lakini kuna nchi ina watu laki moja na 40 ilifuzu sasa tunaweza kipi ndugu zangu.

kutawaliwa ni chaguo zuri, kwani tutakaa tu wao watakua wanabuni teknolojia wanafikilia mambo ya msingi kwaajili yetu kama ilivyo saivi sisi kazi yetu ni kununua na kama hatuwezi kununua tunaingia mkopo tunaweka rehani hata raslimali zetu.

Mbona tumepoteza kila kitu cha muhimu mbegu bora za asili, mifugo yetu kama kuku, ng'ombe nk; saivi kila kitu nivya kisasa, mbegu za mazao ya asili zimeshapotea, zilizopo chache sana nazo ziko mbioni kupotea tulikua na mbegu zetu za mahindi, mtama, alizeti matunda za asili kwasasa hamna kabisa.

Chakula chetu kimetawaliwa na wanga protini mala chache sana, hiki ni chakula cha watumwa mtu aliestaarabika na akaendelea hawez kula mlo huo

ukila tunda 90% ni la kisasa
madawa ya kulevya sio siri yameathiri vijana wengi mpaka serikali imetenga bajeti.
Tumeshindwa ata kubadilisha elimu yetu ifanane na mazingira mwenye taaluma ya afisa kilimo anaendesha bodaboda, mwanahabari anatoa ushauri wa sheria.

Kilimo chetu ni cha jembe la mkono, hata uvunaji wa mazao yetu tunatumia nguvu badala ya akili.
Utamaduni wetu kichomi, ngoma hazina hata ubunifu alafu zile ngoma zimekaa kichawi chawi. Mbona sijawahi kuona mcheza ngoma ambae sio mlevi.
utamaduni wetu unaruhusu ukeketaji.
hata ndoa za utotoni ni asili yetu.
Asili ya mavazi yetu ni kaniki wengine walikua wanavaa mashuka sasa haya ndo mavazi gani na kama nimazuri mbona hamvai.
Tutawaliwe tu tamaduni za wenzetu ni nzuri mavazi yao ya ofisi ni mavazi ya staha, nyimbo zao za kisasa zinaburudisha na zimechangamka zina ubunifu acheni watuuzie utamaduni wao.

Hatuwezi hata kusimamia ujenzi wa bara bara zetu, kuna bara bara inajengwa kiwango cha rami baada ya mwaka haifai kwa matumizi.

Waje waongeze nguvu kwenye uchimbaji wa madini, wabebe yote waondoke nayo watajilike haswaaa tukitaka kudai raslimali watugombanishe tuingie kwenye vita tuuane wenyewe kwa wenyewe.

Wahakikishe tunapata viongozi vilaza kwa kudhamini uchaguzi mkuu wa nchi, viongozi watakaoweza kutuuza mpaka utu wetu wauze hifadhi za taifa wauze hata majengo ya ikulu yabinafsishwe wakusanya kodi wawe wazungu hata ushuru wa mdogo mdogo wakusanye wao. Sisi tumeshindwa jaman ubishi sio mzuri.

Waongeze nguvu kutuzalishia mbegu na vitu vya maabara kama mayai ya kisasa tusiwe na nguvu hata za kupingana nao sasa kama hatuwezi kutunza vyetu tunataka nini?? Unadhani kuna mtu atakuja akupe elimu ya uzalendo au elimu ya kutafta pesa, au elimu ya ubunifu hayo ni mambo ya kujiongeza na kiukweli yametushinda kinachotakiwa tukubali tuwekwe chini wwanaoweza hayo.

Unyanyasaji wa kingono umetawala kila mahali watoto wanabakwa, wengine wanalawitiwa kila siku haya mambo yanaongezeka kila mwaka, kesi zinaishia polisi watu wanamalizana. Tunajua sana kumalizana kimya kimya tunaona ni sawa.

Pia waongeze nguvu kubwa kwenye ubaguzi wa rangi hii itakua mbinu moja safi sana ubaguzi wa rangi unamchango mkubwa sana kwenye kutawaliwa tutazidi kujiona wadhaifu.
KWANINI TUTAWALIWE.
Hatuko tayari kujinasua kutoka katika wimbi la umasikini, maradhi, ujinga, na kutawaliwa hii inadhihirishwa na matendo yetu. Ukiangalia utawala na hali halisi ya jamii inaishi bila kuangalia maendeleo endelevu ya jamii yake.
Jamii imeacha uongozi ufanye lolote wanalojiskia, (waache wanasiasa wafanye wanavyojua wao) hii kauli inaashiria mtu ambae hata akitawaliwa haina shida kwahiyo ni dhahiri tunatamani kutawaliwa. Tunajipa moyo kuwa tunatafta hela, kijana ngoja nikuambie wananchi hawawezi kufanikiwa kama nchi haina mafanikio kiuchumi, kadri uchumi wa nchi unavyodidimia na wananchi wanazidi kudidimia.
Ni dhahili watu wengi tumekaa kwenye siasa kinafiki na sio kutafta namna ya kuisaidia nchi ( tunataka kukuza kipato kupitia siasa) hatuwezi kuupigia kelele uovu tunaogopa kukamatwa.
Mmomonyoko wa maadili ni mkubwa mnooo vijana hawawezi kusikiliza wazee, tumekubali kuishi maisha ya hovyo. Tunahtaji mtu wa kutusimamia.
Tunamuachia Mungu atubadirishie uongozi tunaongea tena kwa kutetemeka (Mungu atusimamie) ni dhahili tunahtaji msaada wa Mungu lakini tumekaa tu tunasubiri miujiza.
Hamna kitu tunakifanya kwa kumaanisha (seriously) tunaishi maisha ya kuigiza igiza au propaganda, tukipata kiongozi mzuri tunamuua alfu tunasingizia mataifa makubwa wamemuua kiongozi wetu pendwa.
Maisha yetu ni mateso kwasababu vyetu tunaona sio bora ila vya wengine sasa hapa tunashihirisha ni namna gani tunahtaji kuwa chini ya watu frani tuwatumikie.
Tumeshaingia kwenye mifumo ya wenzetu na hatuna mpango wowote wakujitoa kwenye mifumo tuliowekewa, hii mifumo inajumuisha mifumo ya malipo, mawasiliano, kiutawala na hizi ndo njia za kututawala kirahisi.
Viongozi wetu wanathibitisha kabisa kuwa tunahtaji kutawaliwa, sisi tumeona kuwa wao ni bora kabisa na wanafaa lakini wanaingia mikataba mibaya na madeni makubwa kwa kujinufaisha wao.
Kuna kivuli kinatudanganya kuwa tuna nguvu, tuna akili, tunauwezo mkubwa, hatupewi nafasi, tunaonewa, tulitawaliwa ndo maana tuko hvi, tunajitahidi sana kuwa visingizio.
Ni kawaida sasa dada zetu kubadilisha rangi zao wanataka kuonekana weupe. hii ni wazi tunadhihirisha kuwa sisi ni dhaifu na kila kitu chetu kibaya mpaka ngozi.
Ukweli unauma na una tabia moja haijalishi utakaa upande wa kuupinga au kuukubali, ukweli utabaki pale pale. Uhalisia wa dunia ni kuwa ni lazima kuwe na mkubwa na mdogo, kiongozi na raia. Sasa hao wadogo, raia, wafanyakazi ndo sisi.

Tumechagua kuwa watu wa chini, tumechagua umasikini, na kuwa wakunyanyaswa, kuteswa na kuendelea kuwa watu duni tusiobadirika, hili sio chaguo letu wote ila wengi wetu matendo yetu yanadhihilisha hivyo, hatuna utayari wa kutafta mabadiliko ya kweli.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom