Tumemchoka sasa Mtangazaji wa TBC1 na TBC Taifa Enock Bwigane abadilike upesi na huu ushamba!

sema umemchoka so tumemchoka we na nani sasa,mi namkubali sana na sema bwigane piga kazi usiskilize Maneno ya mitandao...
 
Binadamu mwenzio unawaita Mimtu! Hii chuki unaitoa wapi?
Mie hapa nilipo matangazo ya mpira nasikiliza TBC .Vituo vingine havioni umuhimu na coverage yao sio kubwa.
kweli mkuu kwenye matangazo ya mpira tbc taifa haikwepeki
 
Enock Bwigane piga kazi.!!! Jana umenitangazia tulipompiga mwarabu.mikia fc wamepagawa.

hakuna redio inayotangaza mpira vzr zaidi ya TBC.mnyobge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Mleta Uzi analo la moyoni. Bwigane hunogesha sana matangazo ya mpira. Huchanganganya lugha tofauti. Kireno, (Obrigado, )kiarabu (wahed) Kinyakyusa (ndaga) kihaya (maweeee) kisukuma (ng'wadila) kikurya (mura mangana) kiingereza.
 
Ahahaaaa! Tusimlaumu, kijana amezoea kukapindisha kamudomo na kuyatamka maneno ya kinyakyusa. Anapata shida sana kuzungumza bila ya kuupindisha mdomo.
 
TBC ni kituo cha taifa tu,lakini sio kituo kikubwa naomba nikusahihishe hapo.
 
Pole ndugu yangu... Hakika umeumia sana..

Karaha kama hizo na nyinginezo nami nilishakutana nazo..

Ila kwangu nimezipatia ufumbuzi wa kudumu kwa kutoangalia TBC TV wala TBC RADIOS...

Sio rahisi kubadilika kwa vyombo hivyo... KAMA HUTAKI KUUMIZA ROHO YAKO, KAA NAVYO MBALI..
 
Bahati mbaya sisikilizi TBC
SIO BAHATI MBAYA MKUU.... NI BAHATI NJEMA HIYO..

UMEBARIKIWA... KUMBUKA KUSIKILIZA UONGO NI KUSHIRIKI UONGO....

UMEEPUKA DHAMBI MKUU, MSHUKURU MOLA WAKO SANA..
 
Kamarada maana yake nini??

Inamaanisha ' mwenza ' katika Kazi zenu zinazofanana au za Tasnia moja na mara nyingine hutumika kama Marafiki hasa mnaoshibana kwa ukaribu wenu. Na ni Kireno hicho ambacho kimetoka katika neno la Kiingereza la ' Comrade '.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…