Tumemsajili kiungo Said Ndemla kuchezea Singida Big Stars kwa miaka miwili

Tumemsajili kiungo Said Ndemla kuchezea Singida Big Stars kwa miaka miwili

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Watu wa Soka,

Leo tumemtambulisha rasmi kiungo bora wa soka hapa nchini, Said Hamis Ndemla, ambaye amesaini kutupatia huduma yake kwa miaka miwili.

Ndemla sifa zake zinajieleza zenyewe. Amekuwa mchezaji ambaye kiwango chake kinapanda siku hadi siku. Atatufaa sana kwenye kufikia malengo yetu ya msimu ujao wa Ligi Kuu 2022/2023.

 
Makolo wanaua vipaji vya wazawa kama Ndemla
Ndemla alijiharibu mwenyewe kwwa kusikiliza sifa za wachambuzi uchwara, oohh, ana nguvu ya kupiga, mwishowe akawa kila mpira anataka kuubutua tu.

Kama mzamiru wanamuita kiungo punda mwishowe kawa chizi, anakaba wee kisha pasi mkaa, si mzamiru yasini yule aliyetoka mtibwa, msimu wake wa kwanza simba pale, national timu tulipoenda kucheza COSAFA kule tukawafunga wa south mpaka kocha wao akakasirika sio yule..

Wachezaji wengi wa kibongo hawana uprofeshenolizm, hawana njaa ya mafanikio, wanalewa sifa, wapi ajib, wapi mo cabaye yule anaujua haswa mpira lakini sasa hivi chaliii,

Kapombe, manula, samata, tshabalala si wanacheza simba, mbona viwango havijafa.

Wachezaji wetu kuvjmba kichwa, kupandisha mabega, cheki msuva na samatta walivyo na njaa ya mafanikio, wengjne hawana.
 
Ndemla kipaji chake ni kikubwa na ana umri mdogo. Bado yuko vizuri sana mkuu.
Ajui kitu uyo dogo kila mada analeta usimba na uyanga.
Said Ndemla kiwango chake kikubwa sana na atawasaidia sana Singida big stars, ninahakika msimu huu wa 2022/2023 Singida piga ua top 3 itawahusu.
 
Ajui kitu uyo dogo kila mada analeta usimba na uyanga.
Said Ndemla kiwango chake kikubwa sana na atawasaidia sana Singida big stars, ninahakika msimu huu wa 2022/2023 Singida piga ua top 3 itawahusu.

Amen mkuu!
 
Hisia zinaniambia kuwa hamtatoboa msimu uanzao hivi karibuni.
 
Mtakuja kuwa timu nzuri sana nyie watu..ila plz tunaomba mturudishie kiungo wetu mnamjua!!!yule mghana
 
Back
Top Bottom