Tumenusurika kuingiliwa na wezi

beevenom

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2017
Posts
313
Reaction score
432
Niende moja kwa moja katka mada, around SAA tisa usiku vibaka/wezi wamevamia nyumbani kwangu. Nashukuru Mungu alikuwa upande wangu hawakufanikiwa kuingia hadi ndani baada ya kusikia milango inafunguliwa kutoka ndani walikimbia.

SOMO;
Kabla ya kulala mtangulize Mungu kama mlinzi wako na pia usiache vifaa hatarishi kama panga, nyundo na mbao nzito, mathalani kwangu kuna vipande vya mbao vya two by six walitumia kunyonga vyuma katika dirisha.

Ahsanteni, nawasilisha
 
Asante sana,yaani mbona usingizi wote umekata. Kuna wakati nimefikiria nitafute manati ya kizungu kama ya general galadudu
 
Ninajaribu kuunganisha dot,juzi nilitoka kidogo baada ya kurudi binti Wa kazi akanambia kuna watu wawili wanaume walifika na kutaka kujua baba na mama kama wapo. Alikuwa mjanja aliwajibu wametoka na wanarudi ndani ya muda mchache. Wakamuuliza jina lake akawajibu jina lake la nini kama wanashida ya baba na mama? Baada ya majibu hayo wakaondoka na Leo ndo wakatia mguu kufanya yao. Kuna haja ya tunaowaacha majumbani kuwaelekeza namna ya kuwatambua watu wasio wema.
 
Pole sana jiandaeni vizuri wanaweza kujaribu tena.

 
Kabisaa,hawa jamaa hovyoo kabisa na hali hii ya uncle magu daaa
 
Jamani hivi manati za kizungu gharama yake ipo vipi na taratibu gani za kufuata ili uipate
 

Wapi huko mkuu?hukuwapiga hata picha wakati wanakimbia?
 

Jipange na jirani zako hapo kiulinzi wanaweza kurudi kihatari zaidi wakafunga mtaa...
 
Poleni sana ashukuriwe Mungu kwa ulinzi wake[emoji120]
 
kwahiyo hao wezi hawakuwa na shida ya kuingia ndani bali walitaka kuiba kupitia dirishani?
Hataivyo nimeshaishi sana na wezi, mida au nyakati wanazopendelea sana kuiba ni nyakati za mvua, alfajiri wakati wengine wakiswali, vipindi vya sikukuu na mara chache jioni.(hii yote inamaana yake).
Vilevile wezi huwa hawaibi kwenye nyumba yenye mtoto mchanga.
 
Pole mkuu ni maeneo gani unaishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…