Tumepoteza Dira na Mwelekeo kama Taifa!

Tumepoteza Dira na Mwelekeo kama Taifa!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
4,526
Reaction score
1,540
Kama Taifa, Watanzania tumepoteza uimara na umadhubuti wa kudai kwa nguvu uwajibikaji.

Kama Taifa, tumeruhusu uongozi mbovu kushikilia dhamana ya kuliongoza Taifa.

Tumefanya hilo kwa hiari yetu wenyewe na kama watu tuliologwa au kupagawa, kila miaka mitano tumewachagua watu wale wale miaka nenda rudi, tukiamini kwa dhati ahadi za tunaowakabidhi hatamu za uongozi kuwa watatuongoza kwa ufanisi, uimara na kwa haki na kutulinda kwa ngao imara katika vita dhidi ya umasikini, ujinga, maradhi na uhalifu.

Lakini tumekubaliana na kauli mbiu nyingi kila siku na hata sasa ya kudai Katiba mpya kama kigezo cha kurahisisha safari yetu ya maendeleo na kujenga jamii imara yenye kutii Sheria na kuwajibika.

Lakini tatizo si Katiba, hata kama tukiiangalia kwa Kiti cha Urais na kudai ana madaraka na nguvu nyingi.

Kwani Raisi kazi yake ni nini?

Ni sisi kama Taifa tumeshindwa kuwajibisha viongozi na kuwalazimisha wawe watii wa sheria, wawe makini kwenye kazi zao na kubwa ni dhamana ya kuongoza Taifa katika safari ya kujenga na kulinda Utaifa na Taifa letu.

Majemedari wetu ni legelege, hawana utashi wa kupigana vita kwa niaba yetu, wanadai silaha hazitoshi, na sisi tunakubali haraka haraka bila kufanya Tathmini ya ujemedari wao na tunaafiki eti lazima tununue silaha mpya!

Kuna maana gani kununua silaha mpya kama majemedari wetu hawana moyo au ari ya kuwa mstari wa mbele kutuongoza vitani?

Silaha mpya zitatulinda vipi kama majemedari hawana mipango na mbinu zinazoeleweka na zenye umakini kupigana vita?

Je tumesahau tulipowakubalia walizike Azimio la Arusha na siasa ya Chama Kimoja kwa kudai Ujamaa na Kujitegemea na Chama kimoja villikuwa matatizo ya maendeleo yetu na vilitufanya kuwa masikini?

Mwaka 1992, majemedari waliuzika Ujamaa na Azimio, wakazika siasa za chama kimoja. Azimio jipya la Matumaini la Zanzibar likazaliwa, mfumo wa mpya wa siasa wa vyama vingi ukazaliwa.

(Tukasahau na kujisahau kuwa majemedari walikuwa wale wale!)

Leo hii, miaka 22 baada ya "Katiba" mpya ya 1992, bado tuko palepale na hatua za kupiga maendeleo zimezidi kuwa fupi na zisizo na uwiano!

Umasikini unashamiri, Ujinga umeongezeka, Maradhi hayaishi, uhalifu (ufisadi, uzembe,ufujaji, kutokuwajibika) umekuwa jambo la kawaida na linapewa enzi na mbaya zaidi tumegeuka kwa Taifa tegemezi na lenye matumizi mabaya ya fedha na deni kubwa la kutisha.

Sasa tujiulize, tujisute, tumelilia rasimu mpya na kuweka vipengele vingi vya upendeleo na lengo kuu tunadai Katiba mpya itaondoa kero na kutustawisha kama Taifa!

Swali na wazo langu la Jumamosi hii ni hili: ni kwa uhakika gani Katiba mpya itatubadilisha kama watu tukaamka na kubaini kuwa majemedari wetu hawatufai ?

Tunanunua silaha mpya ya nini ikiwa Jeshi na majemedari ni wale wale ambao ni wazembe, wabinafsi, wavivu, hawana ufanisi na kila siku kutoa visingizio kuficha udhaifu wao au kulinda maslahi yao?

Iweje tuwaamini majemedari wetu ( angalizo- si CCM pekee, CUF, Chadema na kadhalika) kweli wako tayari safari hii kujitoa mhanga kutuongoza vitani na kulilinda Taifa letu?

Je wakishindwa kuwajibika kwa dhati, tuunde tume au kamati kuchunguza na kuandika Katiba mpya, au kanuni na Sheria mpya?

Jihoji nafsi yako upigapo kura yako: iwe ni kutaka Katiba mpya, Tamisemi 2014 au Uchaguzi Mkuu 2015!
 
Rev. Kishoka;

Amani iwe kwako. Ningependa niulize swali kabla ya kuendelea kuchangia mada. Dira ni kitu au nadharia inayokuongoza kwenye safari fulani. Kabla ya kuanza kuitumia hiyo dira ni lazima hiyo safari ieleweke. Je ni safari gani unayotaka watanzania watumie dira?


Kuanzia 1967 mpaka 1992 kulikuwa na dira na safari ya kujenga taifa la kijamaa. Tatizo lilokuwepo sio Azimio la Zanzibar bali hakuna uwezekano wa kujenga taifa la kijamaa. Hata kama uwezekano wa kujenga taifa la kijamaa upo, itabidi itumike nguvu na umwagaji damu, kitu ambacho wababe dira iliyopotezwa walishindwa au kuogopa kutumia. Ukweli wa mambo ujamaa na Azimio la Arusha yalikuwa ni mambo ya ndoto za Alinacha.

Tukirudi kwenye mada kamili. Moja ya matatizo yanayofanya watanzania kutopata nafasi ya kuchagua viongozi wazuri ni katiba. Kwenye posti yako umesema katiba ya 1992. Ukweli wa mambo ni katiba ya 1977 ndio inayotumika mpaka sasa. Kilichofanyika ni kuondoa CCM au Chama na kuandika vyama vya siasa.

Kujibu swali lako la jumamosi hii: ufanisi wa katiba unatokana na watu wanayoifuata. Katiba peke yake haitoshi iwapo watanzania hawatajenga utamaduni wa mambo mengine yanayoleta maendeleo.
 
Rev. Kishoka,

Kujenga taifa ni neno pana na linaweza kuwa na maana tofauti kwa vipindi na vizazi tofauti. Vilevile kujenga taifa sio kitu kinachoweza kupimika au kutathiminiwa.

Hivyo kuondoa makosa ya kiutawala na uongozi yaliofanyika kwa zaidi ya miaka 50 toka uhuru, Tanzania inabidi ijenge utamaduni wa kufanya initiatives programs ambazo zinaweza kutekelezwa, kupimwa na za muda mfupi
 
Last edited by a moderator:
Zakumi,

Tunaendelea kupotea na kupotezana mwaka huu wa Uchaguzi! ni sawa na mbio za kwenye jungu kuu halikosi ukoko!
 
Back
Top Bottom