Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kwa akili au ufahamu wa haraka haraka ukisikia neno makelele unapata uelewa wa kusikia sauti na mirindimo mbali mbali ambayo huweza kuleta kelele, huenda ikawa sauti kubwa ya mashine viwandani au kelele za mziki nakadhalika.
Lakini kuna kelele nyingine ambazo huenda wengi wetu hatuzijui, nazo si nyingine bali ni kujiingiza katika mambo mengi Sana ambayo yanatuzalishia taarifa mbalimbali ambazo mpaka tunashindwa kuzichakata na kutusababishia usumbufu katika Maisha yetu wala usio wa lazima.
Utakuta mtu ana magroup kibao ya whatsap, huko kwenye Facebook nako ana magroup,huku ana tiktok,pale reels,nyuma smile, juu Snapchat,Chini Instagram, bila kusahau jamiiforums na mitandao mingine kibao. Na yote anataka kuhudhuria Kwa siku moja, mwisho wa siku anakuwa na too much information ambayo bahati mbaya zaidi wala sio health kwasababu hakuna cha maana anachojifunza isipokuwa bla bla bla tu!
Mwisho wa siku tunakuwa na vijana wa ovyo na waliochanganyikiwa, wanatumia Mda mwingi katika hizi platforms lakini hakuna cha maana wanacho jifunza isipokuwa upuuzi mtupu. Mwisho wa siku unazidisha makelele Ku mkichwa na kuleta matatizo ya afya ya akili.
Nashauri kitu kimoja hapa,ebu punguza ushiriki wako katika platforms nyingi na ubakie na chache ambazo hazitaleta makelele Sana katika kichwa chako, afya yako ya akili ni muhimu Sana ndugu zangu.
Hakuna ubaya wa kujaza volume kubwa ya taarifa sahihi kabisa katika kichwa chako lakini ubaya ni kujaza volume za taarifa ambazo sio sahihi na ambazo hakuna unalo jifunza matokeo yake unakuwa na mlundikano mkubwa wa makelele katika kichwa chako.
Natambua ingawa ubongo unaweza kuhifadhi na kuchakata vitabu vyote ambavyo vipo ulimwenguni na usichanganyikiwe wala nini, lakini je hayo ndio matumizi sahihi ya Ubongo wako? Kwanini usiwe na platform chache lakini ambazo kuna kitu utajifunza kila siku na kupunguza makelele kichwani kwako.
Ili ufahamu vizuri dhana nzuri ya makelele kupitia hizi social media na vijukuu vyake, hebu jaribu siku moja kupunguza mahudhurio yako katika hayo mambo na uone jinsi utakavyokuwa free na mwepesi.
Ila Kwa wale ambao tuna platform chache huwezi ona hiyo tofauti kubwa, nawazungumzia wale wenye magroup na platforms mbalimbali ambazo Kwa kila siku lazima ahudhurie huko, huyu akipunguza mahudhurio na kutembelea chache ataona jinsi dunia ilivyokuwa kimya na yenye utulivu wa kutosha.
Binafsi nina platforms tatu ambazo ni jamiiforums, Twitter na Instagram, lakini nahudhuria Sana Twitter na jamiiforums, sasa siku mbili hizi nikaona ngoja nitembelee insta kidogo daah, nikakutana na makelele ambayo wala sikuyatarajia, nikakutana wanaccm wanaombeana Kura,mara Mheshimiwa DC mmoja anamuombea Kura muuza nguo fulani maarufu Sana ambaye inasemwa kazaa naye, mara Wema sijui kammiss whozu, huku uchebe anamuombea Kura mama lishe wake wa zamani maarufu Kama shishi,daah basi nikajikuta kwenye dimbwi la kelele ambazo wala sikutarajia kabisa.
Yaani siku hizi hata kuangalia status whatsap naona makelele Tu! Nimefanya kupotezea.
Vyovyote utakavyoamua kupunguza makelele lakini nakushauri usipunguze makelele ya jamiiforums hakika Yana manufaa na burudani tosha kabisa Kwa ubongo wako.
Natumaini sauti imetosha kabisa!
Ni hayo Tu!