masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
[h=2]
Re: NDALICHAKO: kitu cha ZOMBI[/h]
By asigwa 
Haya ndio watoto wenu wamejaza kwenye karatasi za kujibia mtihani wa kidato cha nne....
Tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele....
Msituko wa kufeli kwa kiwango kinachoshitua kwa vijana wetu, watoto wetu, katika mitihani ya kidato cha nne, ndio kwanza unaanza kueleweka.
Mshituko huu wa zaidi ya 60% ya vijana WOTE, kushindwa mitihani kunakupa mzazi jibu moja tu.
SERIKALI YETU IMESHINDWA KUMWELIMISHA KIJANA WA KITANZANIA.
Hapa hakuna sababu ya kuunda tume wala uchunguzi wakati Wizara ya Elimu. Wizara inayotakiwa kuandaa wataalamu wakesho ikiwa imeshindwa katika majukumu yake ya kimsingi.
Kwa matokeo yaliyoonekana mwaka huu, kuwepo kwa Wizara au kutokuwepo ni sawa tu.
Mbaya zaidi ni hiyo picha ya kiongozi wa juu katika Wizara mama Ndalichako kuonyesha jinsi wanafunzi wanavyochora vibonzo badala ya kujibu maswali ya mitihani.
Ni dhahiri kwamba mwanafunzi hakuandika jibu la mtihani kwa vile HAKUFUNDISHWA namna ya kujibu mitihani.
Lawama ni nyingi na ziko kila mahali lakini huu uozo uko ndani ya Wizara yenyewe ya Elimu.
Kiujumla tatizo hili si tukio la kushtukiza, matatizo ya sekta ya elimu yamejikusanya kwa miaka mingi, na sasa tunaona matokeo yake.
baadhi tu ya matatizo:
Kuliko kuundiwa tume, Wizara yenyewe ikae chini, ijena na mapendekezo ya kuondoa aibu hii ambayo ni upotevu mkubwa wa resource inayohitajika huko mbeke ya safari- resource ya vijana wasomi na wataalam wa baadaye.
Najiuliza, wahandisi wa baadaye kutengeneza barabara watatoka wapi?
Madaktari je?
Wachumi tunao wahitaji?
Waalimu na hata askari wenye utaalam, polisi wenye weledi?
Tusichezee resource hii muhimu, serikali inaombwa kuzingatia kurekebisha tatizo hili.

- Fedha kidogo zinazo tengwa kwa ajili ya elimu kiujumla
- walimu wachache waliopo kukosa motisha kufanya kazi
- kuongezeka sana kwa wanafunzi amabako hakuwiani na huduma ya elimu kwa wanafunzi hao