third eye chakra
JF-Expert Member
- Dec 27, 2023
- 713
- 1,745
🌳TUMESHINDWA KUUMILIKI ULIMWENGU WETU KWA KUUTAMANI ULIMWENGU WA HADITHI.🌳
Ulimwengu wa kweli umetengenezwa katika hadithi isiyo furahisha sana, unaonekana ni ulimwengu ulio jaa mateso ya kila namna, kisha Ulimwengu wa NADHARIA ndiyo umejaa raha za kila namna na umeitwa ulimwengu mpya (PARADISO au PEPONI)
Ulimwengu wa nadharia ndiyo umejenga watu watumwa KIIMANI, kwakua wanatamanishwa kitu ambacho mtamanishaji hajawahi kukiona zaidi ya simulizi katika simulizi zenye sanaa ya ULAGHAI msimuliaji wa Mwanzo katika swali la tukifa tunaenda wapi?
Ulimwengu mpya ni mtazamo ulio jiamini, mtazamo ulio wajaza watu imani kupita kiasi hata kufikia hatua ya kuhitaji Ulimwengu wa kweli ufike mwisho, kwakua ndani yao Kuna matumaini kupita kiasi matumaini ya udanganyifu wa ulimwengu uliopakwa rangi
Kilicho tushinda katika Ulimwengu huu wa kweli ni baada ya kutofungua kurasa zake zote, kwakua tangia tungali wadogo tulifunguliwa kurasa za Ulimwengu mpya wa nadharia na Wale Wenye Kutunga Hadithi za Ulimwengu Huo, kisha Wakatupa Ukomo wa Kurasa za Fikra ili tusisome zaidi ya Kurasa walizitufunilia.
Ulimwengu wa kweli hauwezi kuwa tulivu ikiwa tayari uhuru wake tumeupa Ulimwengu mpya wa hadithi, Ulimwengu ambao tayari umefunga sehemu yetu ya mawazo.
Huu msemo wa "SISI SIO WA ULIMWENGU HUU" umetunyima Akili ya kushindwa kuimiliki dunia kimantiki na kutupa umiliki wa giza wa imani, Lakini Umiliki wa Dunia Umebaki Mikononi mwa Wale Watunzi wa Ulimwengu mpya Wa Nadharia Ambao hata wao hawajawahi kuufikia. tunahitaji mtazamo mzuri kuhusu Ulimwengu wa Kweli, tunahitaji mwanzo ambao unathibitisha kuwapo kwetu si makosa na hata kufa kwetu si dhambi.
Lazima tupate mtazamo wa kimantiki ili tuweze kuunda hatima yetu nje kabisa ya Imani ila ndani kabisa ya ulimwengu wa kweli usio tugawa. Tunahitaji utambuzi utakao tutoa katika Akili bandia za Imani na Kisha Tukaishi katika Msingi Imara wa Asili yetu.
Tunahitaji kumiliki madhaifu/udhaifu wetu na kufanya vyema bila kuusingizia ulimwengu na Shetani. Kuufanya Ulimwengu wa kweli kuwa ni dhaifu na mchafu kuliko Ulimwengu mpya wa hadithi ni kuonesha jinsi ambavyo TUNA IKANDAMIZA ASILI YETU HALISI katika asili ya Imani.
🙏🙏🙏🙏🙏🙏