Tumeshindwa matrekta, basi tujaribu vyerehani

Tumeshindwa matrekta, basi tujaribu vyerehani

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Sekta ya ushonaji wa nguo inafanya vizuri sana China karibu 50% ya uzalishaji wa nguo unafanyika China kupitia viwanda vidogo vidogo.

Serikali na yenyewe ingesaidia sana kupunguza tatizo la ajira kama ingelianzisha somo la ushonaji Kwa elimu ya sekondari. Sekta ya ushonaji nguo ina faida kijamii na kiuchumi kama ifuatazo.

a) Ni ujuzi mrahisi sio mgumu sana unahitaji tu kujua mahesabu ya kawaida hivyo ni rahisi Kwa binti kusoma vyote masomo ya kawaida na ushonaji.

b) Nguo ni hitaji la msingi la binadamu na ingepunguza pia kwenda kuchukua mitumba mitumba iliyovaliwa huko ulaya.

c) Cherehani sio bei kubwa sana bei ya kawaida kabisa rahisi Kwa serikali kuagiza hata cherehani 100000 kila mwaka.

d) Ni fani pendwa hasa Kwa wadada mambo ya mitindo na urembo hivyo wangeifanya Kwa moyo.

E) Ni sehemu ya mazoezi kama unavyojua kushona unafanya mazoezi pale unapunguza hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa hivyo unafanya watu waone faida za mazoezi na waache kuamini kama baadhi ya maradhi yametokana na kulogwa uchawi kumbe ni kutofanya mazoezi tu.

f) Ingepunguza japo kidogo mambo ya udangaji na umalaya maana mabinti wangekuwa busy workshop kushona nguo.

g) Pamba ingepata thamani na watu wengi wangeilima maana ardhi tuliyonayo nahisi Kwa kiasi kikubwa inastawisha pamba

KAMA NITAKUWA SIKO SAHIHI BAADHI YA POINT NIKO TAYARI KUSAHIHISHWA MAANA HAYO NI MAWAZO YANGU BINAFSI SIJAFANYA TAFITI POPOTE WALA KUCHUKUA TAARIFA TOKA CHANZO KINGINE HIVYO NIYAPENDEKEZAYO HUENDA YANAWEZEKANA AU KWA MAZINGIRA YETU NA MIFUMO YA BIASHARA YASIWEZEKANE

download (1).jpeg
download.jpeg
 
Wachina wanatengeneza vipawa tila vidogo vya kulimia, kupalilia, kufukulia viazi shambani why tanzania isiviagize kwa wingi wananchi waachane na jembe la mkono linalolima kidogo? Mabodaboda tu ndiyo yanaingizwa kwa wingi wakati umuhimu wake ni mdogo kuliko zana za kilimo. Hizo pawa tila ni ndogo na bei zake zinaweza kuwa ndogo wakulima wengi wadogowadogo wataweza kuzinunua.
 
Wachina wanatengeneza vipawa tila vidogo vya kulimia, kupalilia, kufukulia viazi shambani why tanzania isiviagize kwa wingi wananchi waachane na jembe la mkono linalolima kidogo? Mabodaboda tu ndiyo yanaingizwa kwa wingi wakati umuhimu wake ni mdogo kuliko zana za kilimo. Hizo pawa tila ni ndogo na bei zake zinaweza kuwa ndogo wakulima wengi wadogowadogo wataweza kuzinunua
Fursa ya biashara Hiyo agiza wewe upate pesa nzuri
 
Wachina wanatengeneza vipawa tila vidogo vya kulimia, kupalilia, kufukulia viazi shambani why tanzania isiviagize kwa wingi wananchi waachane na jembe la mkono linalolima kidogo? Mabodaboda tu ndiyo yanaingizwa kwa wingi wakati umuhimu wake ni mdogo kuliko zana za kilimo. Hizo pawa tila ni ndogo na bei zake zinaweza kuwa ndogo wakulima wengi wadogowadogo wataweza kuzinunua
 

Attachments

  • 1712559691457.mp4
    5 MB
  • 1712559902487.mp4
    4.7 MB
  • 1712559824062.mp4
    5.1 MB
Back
Top Bottom