Tumeshindwa Wapi? Olympic Games Tokyo 2021

Tumeshindwa Wapi? Olympic Games Tokyo 2021

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Kama kuna Medali ambayo Taifa tunastahili basi ni Medali ya vipaji vya kuamini miujiza ya kuvuna tusichokipanda.

Kama tunavyofanya kwenye tozo, badala Mamlaka kuandaa kwanza Wananchi wenye uwezo wa kulipa 'tozo' wao wanaanza na tozo kwanza wakiahidi uwezo wa kulipa utakuja huko mbeleni.

Na ndio vivyo hivyo tunachokifanya hata kwenye maeneo mengine...nina imani bila ya shaka hata Waziri wa Michezo hawezi kubughuhiwa kwa maswali kwa kilichotokea kwani naye atahoji mbona inafanyika hivyo maeneo yote?.

Kama taifa tunaamini tukiendelea tu kushiriki Olympic zote basi kuna siku tutabahatisha Medali, na mpaka sasa tumeshakata miaka 41 tukitoka kapa, labda bado 100 mingine.

Medali 222.png
 
View attachment 1884913
Mkuu tuwapongeze simbu na failuna na gai
 
Kichwa cha mwendawazimu mzee ruksa keshafunga kazi, kwetu kila kitu ni majaribio hatupo siliaz ata kidogo mafanikio bila mipango ni kazi bure hata kama wizara angepewa baba ako
 
Sina mengi ya kuongea ila nakaribisha mawazo. Najua kwa wenye watoto wanapenda watoto wafanye vizuri katika fani mbalimbali kama michezo ikiwa ni pamoja na kupata nafasi (opportunities) za kimataifa kama UEFA, NBA, Olympics, World Championships, Etc. Lakini dalili za nyakati ni mbaya sana kwa nchi yetu.

Hata tuliowategemea kama Hasheem Thabeet alishindwa. Mbwana ndio pekee kaweza katika nchi ya watu 60 million. Kenya wamegundua siri na wanafanya vizuri sana.

Sisi hata Umiseta na Umishumta zilifutwa kwa kipindi fulani bila sababu maalum. Je kuna matumaini kweli ya Tz kuibuka kama nchi ya wachezaji wazuri wa kimataifa?

sketch-1628418519253.png

sketch-1628418464429.png
 
Michezo ni starehe na starehe ni gharama. Uwekezaji kwenye michezo ni lazima,hakuna njia ya mkato kwenye kufanikiwa michezoni Kama pesa haitotumika
Nalog off
 
Tatizo hatupo siriazii kabisaa,kambi mbovu hawana vifaa
I agree kabisa. Na kuna vijana wenye nguvu na uwezo wa kupambana lakini kama mtu hata hela ya chakula inamsumbua na hapati sapoti hayo mengine je? Nchi za wenzetu wanatenga fungu kabisa.
 
Michezo ni starehe na starehe ni gharama. Uwekezaji kwenye michezo ni lazima,hakuna njia ya mkato kwenye kufanikiwa michezoni Kama pesa haitotumika
Nalog off
Michezo ni starehe inayoingizia vijana na mataifa madola in millions. Angalia west africa jinsi ilivyobadilisha nchi ikiwa ni pamoja na Nigeria, Ghana nk. Sisi population inakuwa kubwa tu ila tunabakia na diamond kwa nyimbo na Samatta, na Marehemu Mengi in business. Kwa idadi ya WaTz ilitakiwa kuwa na wawakilishi wengi duniani in sports, music, business, nk.
 
Ni aibu sana kwa kweli hayo mashirikisho ya michezo sijui yanafanya nini Kwa kweli! Tuendelee kusubiri ya kutokuwa na wawakilishi au kuwa nao wachache kwenye All African Games
Nalog off
 
Sina mengi ya kuongea ila nakaribisha mawazo. Najua kwa wenye watoto wanapenda watoto wafanye vizuri katika fani mbalimbali kama michezo ikiwa ni pamoja na kupata nafasi (opportunities) za kimataifa kama UEFA...
Kwani Tanzania ilienda kushindana ?
 
Tumepeleka washiriki wachache sana. Walioenda wamejitahidi sana wote wamekimbia marathon na marathon ni moto. Kati ya michezo migumu sana ni long distance marathon.

Sijui wenye mamlaka ya michezo Tanzania wamelala? Hata hawa waliofanikiwa kwenda wanaonekana ni jitihada zao wenye bila msaada wowote kutoka kwenye mamlaka.

Walioshiriki kuiwakilisha Tanzania hongereni sana ingawa hamkushinda medali lakini mmeonyesha kwamba nyie ni world class Olympian athletes 👏👏
 
Back
Top Bottom